Picha na Habari na Dixon Busagaga 
wa Globu ya Jamii,Moshi 
TIMU ya Machava FC ya mkoani Kilimanjaro maarufu kama mnyama mkali inayoshiriki ligi ya mabingwa wa mikoa (RCL) imeendelea kumiminiwa misaada kutoka kwa wadau mbalimbali safari hii benki ya Azania tawi la Moshi ikijitosa kuisaidia Jezi pamoja na suti kwa ajili ya safari. 
 Kutolewa kwa msaada huo unaendelea kukoleza chachu ya ushindi kwa timu hiyo katika mchezo wao dhidi ya Stand United ya mkoani Shinyanga utakao pigwa katika dimba la chuo kikuu cha ushirika na biashara cha mjini Moshi MUCCoBS weekend hii. 
 Akikabidhi msaada huo kwa mkuu wa mkoa wa mkoa wa Kilimanjaro, Mhe Leonidas Gama, meneja wa Benki ya Azania Tawi la Moshi, Hajira Mmambe amesema kama wadau wa michezo wamevutiwa na mafanikio ya timu hiyo huku akiahidi kuwepo uwanjani katika kila mchezo wa timu hiyo hata nje ya mkoa wa Kilimanjaro. 
 Mmambe amesema msaada huo ni mwanzo wa kile walichodhamiria kukifanya kama wadau na wapenda maendeleo kupitia michezo kuhakikisha sifa ya mkoa wa Kilimanjaro katika michezo inarejea kama ilivyokuwa hapo awali. 
 Amesema pamoja na kuwa wageni katika mkoa wa Kilimanjaro, watahakikisha wanakuwa sehemu ya mafanikio ya timu hiyo huku akiahidi kuongozana na timu hadi Shinyanga katika mchezo wa marudiano utakaopigwa Jumatano ijayo. K
wa upande wake mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama, mara tu baada ya kupokea msaada huo aliwataka wachezaji wa timu hiyo kutambua dhamana walionayo mbele ya wakazi wa Kilimanjaro na kuahidi kutoa shillingi 300,000 kwa kila goli litakalofungwa katika mchezo wa mwishoni mwa wiki.. 
 Machava FC imefanikiwa kuingia hatua nyingine kufuatia maamuzi ya shirikisho la soka Tanzania TFF kuipatia ushindi baada ya timu ya Mpwapwa stars kushindwa kufika katika uwanja wao wa Jamhuri kwa ajili ya mchezo wa marejeano.
 Wachezaji wa timu ya Machava akatika muonekano mpya.
 Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa Machava pamoja na wafanyakazi wa Benki ya Azania tawi la Moshi mara baada ya benki hiyo kukabidhi jezi na suti za safari kwa timu hiyo..
 Meneja wa benki ya Azania tawi la Moshi Hajira Mmbela akikabidhi jezi kwa ajili ya timu ya Machava inayoshiriki ligi ya mabingwa wa mikoa.
 Meneja wa benki ya Azania tawi la Moshi Hajira Mmbela akikabidhi jezi kwa ajili ya timu ya Machava inayoshiriki ligi ya mabingwa wa mikoa.
 Katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro Dk Faisal Issa akitangaza majina ya kamati ya kuisadia timu ya Machava katika uwanja wa chuo kikuu cha ushirika na biashara MUCCoBS.
 Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akizungumza na wadau na viongozi wa chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro pamoja na wachezaji wakati wa kutambulisha kamati ya kuisadia timu hiyo.
Wachezaji pamoja na mashabiki wa Machava.
Wafanyakazi wa benki ya Azania wakiwa uwanja wa chuo kikuu cha Ushirika na Biashara MUCCoBS wakifuatilia mazoezi ya timu ya Machava inayoshiriki ligi ya mabingwa wa mikoa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 14, 2013

    This is what we call morbid obesity, when the BMI is > 40, and one clever clog thought Dar needs KFC!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...