Waziri wa Fedha Dk. William Mgimwa akiongea jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Kiarabu kwa Maendeleo ya Afrika (BADEA) Abdelaziz Khelef wakati wa utiaji saini wa makubaliano ya kuisaidia Tanzania dola za kimarekani 450,000/= kwa ajili ya miradi ya maji katika maeneo ya Mugango, Kiabakari na Butiama mkoani Mara na dola za kimarekani 300,000/= kwa ajili ya msaada wa kiufundi kwa ajili ya kusaidia kituo cha Hesabu cha Pan African kilichopo chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Utiaji saini huo ulifanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha Dk. William Mgimwa (kushoto) akimshukuru Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Kiarabu kwa Maendeleo ya Afrika (BADEA) Abdelaziz Khelef mara baada ya kumalizika utiaji saini wa makubaliano ya kuisaidia Tanzania dola za kimarekani 450,000/= kwa ajili ya miradi ya maji katika maeneo ya Mugango, Kiabakari na Butiama mkoani Mara na dola za kimarekani 300,000/= kwa ajili ya msaada wa kiufundi kwa ajili ya kusaidia kituo cha Hesabu cha Pan African kilichopo chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Utiaji saini huo ulifanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe akipongeza Waziri wa Fedha Dk. William Mgimwa (kushoto) mara baada ya kumalizika kwa utiaji saini wa makubaliano ya kuisaidia Tanzania dola za kimarekani 450,000/= kwa ajili ya miradi ya maji katika maeneo ya Mugango, Kiabakari na Butiama mkoani Mara na dola za kimarekani 300,000/= kwa ajili ya msaada wa kiufundi kwa ajili ya kusaidia kituo cha Hesabu cha Pan African kilichopo chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Kuli ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Kiarabu kwa Maendeleo ya Afrika (BADEA) Abdelaziz Khelef.
Baadhi ya maofisa kutoka Benki ya Kiarabu kwa Maendeleo ya Afrika (BADEA) wakifuatilia utiaji saini wa makubaliano ya kuisaidia Tanzania dola za kimarekani 450,000/= kwa ajili ya miradi ya maji katika maeneo ya Mugango, Kiabakari na Butiama mkoani Mara na dola za kimarekani 300,000/= kwa ajili ya msaada wa kiufundi kwa ajili ya kusaidia kituo cha Hesabu cha Pan African kilichopo chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Utiaji saini huo ulifanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.Picha na Anna Nkinda - Maelezo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 19, 2013

    Ankal Michuzi,
    Naomba hii usiitupe kapuni ni angalizo tu:

    Dola za kimarekani 300,000 zaandikwa $300,000 ile alama mbadala ilotumika katika maelezo /= ni kwa minajili ya Shillingi. Sidhani ni sahihi kuandika Sola za kimarekani 300,000/= hapana.

    Ahsante

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 19, 2013

    Naomba nifanye marekebisho kidogo kuhusu takwimu Za kilichosainiwa Leo. Mkopo wa mradi wa maji mugango, kiabakari&butiama ni Saudi fund USD 15 million na BADEA USD 10 million. Grants of USD 450000 Kwa ajili ya wizara ya maji, na USD 300000 kwa ajili ya pan African center for mathematics UDSM. Picha ya juu anayeongea Na mhe Dr mgimwa ni Eng. Al Bassam, managing director wa Saudi fund

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 19, 2013

    hapa naona mwandishi kamalizia na alama ya shilling(/=)kwenye viwango hivyo vya dola zilizo orodheshwa tafadhali rekebisha hilo tuweze kufahamu kiwango halisi

    ReplyDelete
  4. Hizi pesa ukiziweka kwa kitanzania ni nyingi sana, hasa hasa kwa sisi watu wa dola moja kwa siku. Ukweli ni kuwa hao jamaa wanaopokea hiyo mikataba wana pesa kuliko hizo pesa tunazopewa/kukopeshwa. Ukiwapa wananchi hizo pesa wafungue biashara, utawatoza ushuru kutoka kwa biashara zao, wao watafungua maduka na biashara nyingine, ambazo kutokana na faida wanazopata wataweza kulipa huo ushuru na kuishi maisha mazuri. Kutokana na kuwa kuna watu wamefungua biashara nyingi waliokuwa hawapati huduma nzuri basi watapata, watalipia na biashara itakuwa nzuri.
    Hivi hii logic ndogo mbona haitumiki kwetu?
    Hii ndio dhana asilia ya uchumi katika nchi zote. Usiishie(kama kiongozi) kukusanya ushuru wakati huwajibiki, kwa sababu uchumi utadondoka.
    Uchumi sio jukumu la walalahoi ambao hawana uwezo wa kuficha pesa zao kwa mabank ya uswis. Ni jukumu la sisi wote kuwa wawazi kwa kipato chetu na jinsi tunavyotengeza pesa, hata serikali nayo pia inabidi iwajibike katika hili.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 20, 2013

    Mdau aliyeandika kuwagawia hizo pesa wafanyie biashara ili watumie kulipa ushuru na kuongeza pato la taifa amewaza vema sana .Ila watanzania karibu wengi hela ya kupewa hata kama ni mkopo , utasikia mtu ameongeza mke, mara kanunua kanga za kufunda mwali, n.k

    Wa TZ sote ni mafisadi tukipata mwanya. Tusibeze wanoficha pesa uswiss nao walipata nafasi ya kufanya hivyo.

    Watanzania tujifunze uzalendo wa kujali rasilimali za taifa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...