Benki ya NMB imeendelea kuwa kinara katika kubuni na kuboresha huduma mbali mbali za kibenki, ili kuwawezesha wateja wake kupata unafuu na urahisi wa upatikanaji wa huduma za kibenki nchini Tanzania. Katika kulizingatia hili mwishoni mwa wiki Benki ya NMB ilizindua akaunti ya Chap Chap ambayo kusudi kubwa ni kuwafikia wananchi wote kule waliko na kuwafungulia akaunti zao.Kikubwa zaidi ni kwamba mteja ataweza kufungua akaunti papo hapo na kupata kadi yake ya kutolea fedha ndani ya dakika kumi

• Mambo muhimu zaidi ambayo mteja wa Chap Chap anaweza kufaidika nayo ni pamoja na:
• Kuona salio la akaunti yako popote ulipo
• Kuweka fedha na kutoa fedha kwa mawakala wa M- pesa
• Kutuma fedha kwa wasio na akaunti mahali popote nchini kwa kutumia huduma ya Pesa Fasta
• Kununua vocha za muda wa maongezi kutoka kwenye mtandao wowote wa simu
• Kuchukua fedha hadi shillingi 1.000,000/= kutoka kwenye ATM

Mheshimiwa waziri wa fedha Dk William Mgimwa akichukuliwa alama za vidole na Ofisa mauzo ya Nje NMB Abdul Kandoro mara baada ya uzinduzi rasmi wa NMB chap chap akaunti mwishoni mwa wiki mkoani Dodoma

Ofisa mtendaji mkuu wa benki ya NMB Mark Wiessing akimshukuru mheshimiwa waziri wa fedha Dk William Mgimwa mara baada ya kuzindua akaunti ya NMB Chap chap .

Sehemu ya maofisa na wageni waalikwa kwenye uzinduzi huo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...