Mkuu wa Idara ya Uendelezaji Biashara ya M-pesa
Jackson Kiswaga akionesha jinsi M-pesa inavyoweza kuboreshwa kukidhi mahitaji
zaidi ya bodi ya mikopo ya elimu ya juu ambayo huitumia huduma hiyo kama njia
kuu ya kukusanyia ada ya maombi ya mkopo tangu mewaka 2010. Wanaomuangalia ni
Meneja Uhusiano wa Mambo ya Nje wa Vodacom Salum Mwalim (kulia) na Naibu
Mkurugenzi wa Tehama wa bodi Cuthbeth Simalenga. Vodacom ilitembelea makao
makuu ya bodi hiyo jana kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa taasisi hizo mbili.
Mkuu wa Idara ya Mawasiliano, Habari na Elimu
kwa Umma wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Cosmas Mwaisbwa akifafanua jambo
wakati wa kikao baina ya bodi na kampuni ya Vodacom Tanzania kuangalia namna ya
kuimarisha na kubioresha zaidi uhusiano wa biashara baina ya taasisi hizo
mbili. Wengine pichani kutoka kulia ni Meneja Uhusiano wa Mambo ya Nje wa
Vodacom Salum Mwalim na Naibu Mkurugenzi wa Tehama wa bodi Cuthbeth Simalenga,
Na Mwandishi wetu.
Bodi
ya mikopo ya elimu ya juu nchini - HESLB imesema huduma ya M-pesa
inayowawezesha waombaji wa mikopo ya elimu juu kwenye bodi hiyo kulipia ada ya
uombaji kwa kiasi kikubwa imesaidia kurahisisha uendeshaji ikwemo usimamizi na
ufuatiliaji wa malipo hayo.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa Bodi
ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini Bw. Cuthbeth Simalenga wakati wa kikao cha
urafiki mwema kati ya uongozi wa Bodi na Kampuni ya Vodacom kilichofanyika
makao makuu ya bodi hiyo yaliyopo Msasani Jijini Dar es salaam kwa lengo la
kuimarisha uhusiano wa taasisi hizo.
Bw.
Simalenga amesema bodi hiyo ilianza kutumia huduma ya M-pesa kwa malipo ya ada
ya maombi miaka mitatu iliyopita na kwamba tangu wakati huo huduma hiyo imekuwa
ikiimarika na kutoa tija zaidi kwa upande wa uendeshaji wa shughuli za uombaji
wa mikopo.
"Kwa
miaka mitatu sasa tumekuwa tukitumia huduma ya M-pesa kukusanyia ada za malipo
ya maombi ya mikopo, kwa sasa waombaji wote wanatumia huduma hii na tumekuwa
tukiboresha mifumo yetu ya ndani mara kwa mara kukabiliana na changamoto za
hapa na pale zinazojitokeza."Alisema Bw. Simalenga
Zaidi
ya waombaji 50,000 wakiwemo waombaji wapya na wale wanaaondelea na elimu ya juu
hutuma maombi ya mikopo kwenye bodi hiyo kwa mwaka, na wote kwa sasa
wanatumia huduma ya M-pesa kulipia ada ya malipo ya maombi ambayo ni Sh 30,000.
Bw.
Simalenga amesema changamoto kubwa inayowakabili kwa sasa katika mfumo huo wa
malipo kuwa ni uaminifu wa waombaji hasa wanafunzi ambao baadhi yao hulalamika
kushindwa kulipia au na kudai kutaka kurejeshewa fedha zao wakati huohuo wakiwa
tayari wameshakamilisha mchakato wa uombaji na fedha hizo kupaswa kutumika kama
ada ya uombaji.
"Wamekuwepo
baadhi ya waombaji ambao wamekuwa wakisababisha usumbufu wa hapa na pale kwa
kutuma maombi na kufanya malipo baadae wanarudi na kupiga simu Vodacom kudai
kurejeshewa fedha zao kwa madai kuwa wamebadili mawazo ya kuomba mkopo wakati
sio kweli." Aliongeza Bw. Simalenga
"Tunaomba
waombaji wote na umma kwa ujumla kutambua kuwa mamlaka ya kurejeshewa fedha Sh
30,000 ya ada ya uombaji yapo nje ya Vodacom, hilo ni la Bodi na kwamba sasa
tumeweka utaratibu wa kurudisha fedha hizo mwishoni mwa zoezi la uombaji
tukizinagtia taratibu za kiuhasibu za bodi baada ya kujiridhsiha kuwa
utambulisho wa muamala (Transaction ID) wa mwombaji haijatumika kuendelea na
zoezi la uombaji mkopo."Alifafanua
Aidha
ametumia nafasi hiyo kuzungumzia uhusiano wa bodi na kampuni ya Vodacom ambao
amesema una kila nafasi ya kuwa imara zaidi huku akiishauri Vodacom kuongeza
ubunifu zaidi kwenye mfumo wa malipo ya M-pesa ili mfumo huo uweze kuwa na tija
zaidi kwa wadau wake hasa wabia wakubwa.
"Vodacom
imekuwa karibu na sisi na bado kuna fusra zaidi ya ubunifu kwenye huduma hii
itakayotoa tija zaidi kwetu."Alisema Bw Simalenga na kuongeza
"Tunafurahia uhusiano wetu wa kibishara kwa kipindi chote hiki kwani
tumepata ushirikiano mkubwa kutoka kwa Vodacom pekee hivyotumejikuta tukiwa na
M-Pesa pekee."
Kwa
upande Mkuu wa Idara ya Ukuzaji Biashara ya M-pesa wa Vodacom Bw Jackson
Kiswaga amesema kiasi cha Sh. Bilioni Moja na Milioni Mia Nne kinapitia katika
mfumo wa M-pesa kama ada ya uombaji wa mikopo kila mwaka.
"Tumekuja
kubadilishana uzoefu na wenzetu juu ya uhusiano wetu unaotuunganisha kupitia
huduma ya M-pesa, bodi hii imekuwa sehemu muhimu kwetu kibiashara na
tunatarajia kuimarisha zaidi huduma hii siku zijazo."Kiswaga aliwaambia
waandishi wa habari wakati wa ziara hiyo.
Kiswaga
amewakumbusha waombaji wa mikopo wa bodi hiyo ya elimu ya Juu kuendelea kuitumia
huduma ya M-pesa katika kulipia ada ya uombaji kwa kuwa ndio njia rahisi na ya
kuaminika zaidi kwao inayowapunguzia gharama za usafiri,muda na usumbufu.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Urejeshaji Mikopo wa Bodi hiyo Bw. Juma Chagonja
amesema bado zipo fursa nyingi bodi inazoweza kuzitumia kwenye huduma ya M-pesa
na kuwataka wananchi kuvuta subira kuona mambo mazuri zaidi siku chache zijazo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...