Katibu wa Chama cha Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola (CPA) Tawi la Tanzania Dkt Thomas Kashilillah akimpa muhtasari Mwenyekiti wa CPA Tawi la Tanzania Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb) wakati wa kikao cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika kwenye Ofisi ya Bunge mjini Dodoma mapema leo.
Afisa Dawati wa CPA Ndugu Saidi Yakubu akiwapitisha wajumbe kwenye dondoo za taarifa ya kikao kilichopita.
Mwenyekiti wa CPA Tawi la Tanzania Mhe. Mussa Aaazn Zungu akiendesha kikao cha Kamati Tendaji.
Mhe. John Shibuda (kulia), Mjumbe, akichangia kwenye kikao hicho ambacho kinafanya maandalizi ya kumchagua Mwenyekiti wa CPA tawi la Afrika.
Makamu Mwenyekiti CPA Tawi la Tanzania Mhe. Beatrice Shelukindo akifafanua jambo la kimkakati.
Mjumbe wa Kamati Mhe. Zainab Vulu akielezea uzoefu wake ndani ya CPA.Picha na Prosper Minja - Bunge.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...