Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wakazi wa jijini Tanga, wakati alipofika eneo la Pongwe jijini Tanga leo Juni 21, 2013 kwa ajili ya kuweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa Viwanda katika eneo hilo maalum la Uwekezaji la Tanga Economic Corridor Sez, linalosimamiwa na Wawekezaji kutoka nchini Korea Kusini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Viwanda, katika eneo maalum la Uwekezaji la Tanga Economic Corridor Sez, wakati wa sherehe hizo zilizofanyika leo Juni 21, 2013 jijini Tanga. Kushoto kwa Makamu ni Mwenyekiti wa Bodi ya Tanga Economic Corridor Ltd, Chris Incheul Chae.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa, Mwenyekiti wa Bodi ya Tanga Economic Corridor Ltd, Chris Incheul Chae na viongozi wengine kwa pamoja wakifurahia baada ya Makamu kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Viwanda, katika eneo maalum la Uwekezaji la Tanga Economic Corridor Sez, wakati wa sherehe hizo zilizofanyika leo Juni 21, 2013 jijini Tanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 21, 2013

    TANGA NYUNDOasi KUBWA!

    Si mchezo heshima ya kuwa na viwanda inarudi ndio mwanzo wake huu.

    Tunataka na Bandari ipanuliwe kwa kuwa nchi inakosa mapato makubwa sana wakatiuwezo unaotumika ni mdogo saana.

    World Bank na IMF wamesha toa Report zinazoelezea umuhimu huo kama itaboreshwani wazi tunaweza kiugaragaza Jamhuri ya Kenya na MOMBASA PORT yao hata LAPSSET ya LAMU inayojengwa kwa kushirikiana na Kenya, Ethiopia na South Sudan hazitaweza kufua dafu kwa Bandari nne za Tanzania zikiboreshwa na mpya hiyo ya Bagamoyo kujengwa:

    1.TANGA PORT.(kuboreshwa)
    2.MTWARA PORT.(kuboreshwa)
    3.DAR ES SALAAM PORT.(kuboreshwa)
    4.BAGAMOYO-MWAMBANI PORT.(mpya)

    Niwazi mtiririko wa mizigo ya Afrika ya Mashariki kwenda RWANDA, BURUNDI, UGANDA na CONGO-DRC italazimika kuchagua kati ya Bandari hizo hapo juu 4 za Tanzania!

    TENA ILI KU ADD VALUE BANDARI MBILI ZA MTWARA NA TANGA ya MTWARA INAJENGWA KWA KUWEKEWA GAS REFINERY (MTAMBO WA KUSAFISHA GESI ASILIA) HUKU YA TANGA INAJENGWA NA OIL REFINERY KWA AJILI YA KUSAFISHIA MAFUTA!

    TANZANIA KWA MITAJI HIYO HAPO JUU KIMAENDELEO NA KASI YA UCHUMI WATATUSHIKIA WAPI?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 21, 2013

    Mdau hapo juu umeongea ni kweli kabisa watatushika wapi?Hakuuuna, ila tabu hao wenye nchi wanasikia basi? Mh haya ebu ngoja tuone mana nchi Tz siasa zake1?!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 22, 2013

    Mzee Omar Nundu, ahsante sana kwa kutimiza ahadi yako ya kuiinua Tanga. Japo wachumia tumbo walikufanyia fitna, lakini sisi wananchi tunafahamu na kuheshimu UZALENDO WAKO.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...