Mfanyabiashara maarufu mjini Singida, Mushi Kimboka (aliyweshika maiki) akitoa taarifa yake kwa mjumbe wa halmashauri kuu CCM (NEC) taifa manispaa ya Singida, Hassan Mazala(aliyevaa miwani) juu ya ujenzi wake wa hotel ya Chemuchemu Park iliyoko katika kijiji cha Manguanjuki nje kidogo ya mji wa Singida.
Mkurugenzi mtendaji wa hotel ya kitalii ya Stanley Motel, Eward Malya maarufu kwa jina la Hali Ngumu akitoa nasaha zake kwenye hafla ya uzinduzi wa hotel ya Chemuchemu park iliyopo kijiji cha Manguanjuki nje kidogo ya mji wa Singida.Hali Ngumu amewataka wafanyabiashara kufanya biashara halali kwa bidii na kisha wabane matumizi kwa madai kuwa 'hali ni ngumu'.
Mjumbe wa halmashauri kuu CCM (NEC) taifa manispaa ya Singida,Hassan Mazala akizindua rasmi hotel ya Chemuchemu Park iliyopo katika kijiji cha Manguanjuki nje kidogo ya mji wa Singida.
Wanachama wapya wa CCM baada ya kukabidhiwa kadi juzi na mjumbe wa halmashauri kuu CCM (NEC) taifa Hassan Mazala (hayupo kwenye picha).
Kikundi cha burudani cha kijiji cha Manguanjuki kikitoa burudani wakati wa uzinduzi wa shina la wakereketwa wa CCM katika hotel ya Chemuchemu park.
Mjumbe wa halmashauri kuu CCM (NEC) taifa manispaa ya Singida,Hassan Mazala (wa tano kushoto mbele) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa hotel ya Chemuchemu park iliypo kijiji cha Manguanjuki nje kidogo ya mji wa Singida.(Picha zote na Nathaniel Limu).
Edward Malya ni marauding kwa jina la "MALIYATABU".Nawapongeza Nambari One kwa kuvuna Wanachama Lukuki
ReplyDelete