Baadhi ya Viongozi wa Chadema na wakazi wa Arusha wakiwa katika mazishi ya marehemu Judith William Moshi aliyekuwa kiongozi wa CHADEMA kata ya Sokon 1,Judith aliuawa katika shambulio la bomu lililotokea katika mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi mdogo wa madiwani,soweto Arusha.
Baadhi ya Wabunge ,Viongozi wa Chadema na wakazi wa Arusha wakiwa katika ibada ya mazishi ya marehemu Judith William Moshi aliyekuwa kiongozi wa CHADEMA kata ya Sokon 1 jijini Arusha,ibada ya mazishi ilifanyika katika kanisa la KKKT Usharika wa Sokoni 1 na kuzikwa katika makaburi ya Sokon 1.Judith aliuawa katika shambulio la bomu lililotokea katika mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi mdogo wa madiwani,Soweto Arusha.
Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema (kulia) na Mbunge Grace Kiwelu (viti maalumu Moshi) wakiwa mstari wa mbele na wabunge wengine wakiongoza kubeba jeneza la Marehemu Judith William Moshi aliyekuwa kiongozi wa CHADEMA kata ya Sokon 1 jijini Arusha,ibada ya mazishi ilifanyika katika kanisa la KKKT Usharika wa Sokoni 1,Judith aliuawa katika shambulio la bomu lililotokea katikamkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi mdogo wa madiwani,soweto Arusha.
Baadhi ya viongozi wa CHADEMA wakimpumzisha Judith katika nyumba yake ya milele, Judith William Moshi alikuwa ni katibu wa CHADEMA kata ya Sokon 1 jijini Arusha na aliuawa katika shambulio la bomu lililotokea katika mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi mdogo wa madiwani,Soweto Arusha.
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe. Joseph Mbilinyi (SUGU) wakiweka udongo katika kaburi la Marehemu Judith William Moshi aliyekuwa katibu wa CHADEMA kata ya Sokon 1 jijini Arusha,Judith aliuawa katika shambulio la bomu liliotokea katika mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi mdogo wa madiwani,Soweto Arusha.
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akiweka shada la maua katika kaburi la Marehemu Judith William Moshi aliyekuwa katibu wa CHADEMA kata ya Sokon 1 jijini Arusha,Judith aliuawa katika shambulio la bomu liliotokea katika mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi mdogo wa madiwani,Soweto Arusha.
na wapa pole wanafamilia.
ReplyDeletemkaemkijua hao wakishazika ndio bye byeeee hawarudi nyuma tena. familia inapata pigo kwa mtu kujitakia mwenyewe leo hii wale wote waliokuwa wanaishi kwa mikono ya huyu mama ndio basi tena, tujufunze kutokana na makosa jamani
poleni wana familia. hao viongozi wa chadema wote ni wanafiki kama kweli walikuwa wanania njema na wananchi wao kwanini walikimbia na kujificha??? siwangejitokeza kupigania haki ya wanachadema wenzao.... KWELI KUNAMSEMO USEMAO KILA NAFSI ITAONJA MAUTI LAKINI SII KWA KUJITAKIA JAMANI....
ReplyDeleteKutokana na msiba huu kuna mambo mengi ya kujifunza.watanzania inabidi tuwe makini kwenye kipindi hichi cha mpito.mengi yametokea,je ni wapi tunapokosea!kwanini yatokee sasa?.amani tuliyonayo ndo inatufanya twende ata kwenye mikutano.LINDA AMANI...RIP JUDITH
ReplyDeleteHawa CDM sio wanafiki..wao hawakutaka kukamatwa kama panzi. walienda kujipanga kwa kukamatwa au style ya kujisalimisha.
ReplyDeleteWao wao waliona kila anayeshuka kwenye kanta ( jukwaa) anakamatwa,ikabidi wapitie upande mwingine ili wasikamatwe.
Walijua kuwa wao ndio waliokuwa wakitafutwa.
Mimi sio mwanasiasa ila natoa maoni tu.
Nashindwa kuielewa hii serikali ya sasa. Yaani imeshindwa kutuma hata mwakilishi kwenye haya mazishi!!!
ReplyDeleteUtaifa ukuwapi?
Poleni sana wana CDM. Mmeshambuliwa na Kuuawa kwa Unyama wa kigaidi. Aliyefanya haya ni mtu mwovu.
ReplyDeleteSemeni yote lakini hakuna mwenye haki ya kutoa roho ya mwenzake. Siku viongozi wa leo wakijikuta ni wapinzani nadhani wataanza kulalamikia siasa za visasi ila kwa sasa inaonekana ni sawa watu kuuwawa!!
ReplyDeleteWANAOISHI KWA UPANGA WATAKUFA KWA UPANGA - BIBLIA TAKATIFU.
ReplyDeleteBIBLIA TAKATIFU INATUAMBIA "THOSE WHO LIVE BY THE SWRD WILL PERISH BY THE SWORD". CHADEMA WAACHE KUCHOCHEA FUJO LA SIVYO WATAJUTA!
ReplyDeleteHizi siasa zinatupeleka pabaya sana sasa; viongozi wetu kuweni makini sana; mnajitafutia mnayoyataka kwa kumwaga damu na kupoteza maisha ya hao hao ambao eti mnadai mnawatetea maslahi yao; haiingii akilini hata kidogo kwa sisi wengine.
ReplyDeleteIfike pahala muone hata haya(soni) japo kidogo.
Poleni sana wafiwa; muwe na subra katika kipindi hiki kigumu kwenu, na namwomba Mwenyezi Mungu amjalie pumziko la milele marehemu wetu.
Mmmmmh! Naona watu wana comment kama vile wana ushahidi chadema ndo waliorusha hilo bomu au ndio wenye makosa. Nadhani tuwe wapole wakti uchunguzi unaendelea. R.I.P Judith!
ReplyDelete