NAIBU Waziri wa Sayansi na Tekinolojia January Makamba,anatarajia kuwa mgeni rasmi, katika shindano la umsaka malikia wa Redd's Miss Tanga 2013 linalotimua vumbi katika uwana wa Mkwakwani Mkoani hapa.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini hapa jana, Mkurugenzi wa DATK
Intertainment Asha Kigundula alisema, maandalizi yamekamilika
kilichosalia ni muda kufika na mrembo kuwekwa hadharani.
“Nashukuru
mungu mambo yameenda sawa, kilichokuwa kimesalia ni kumtangaza mgeni
rasm na nashuuru tumeisha mpata tayari mh;Makamba na hakuna kingine, cha
muhimu mungu atuongoze katika shughuli yetu esho mambo yaende
sawa,”alisema Kigundula.
Aidha
Kigundula alisema, ameamua kutoa zawadi ya fedha taslimu kwa warembo na
sio vitu ili warembo wake waweze upata fursa ya ujichagulia kitu cha
kununua wenyewe uliko ununuliwa na kudai uwa mshindi wa kwanza ataondoka
na kitita cha sh 500,000, wa pili sh 300,000 na wa tatu sh 250, 000.
Huku
wa nne na tano wakipata sh.200, 000 kila mmoja na warembo wengine
watakaosalia watapata kitita cha sh 100,000 kila mmoa kama kifuta jasho
pamoja na zawadi kwa mrembo mwenye nidhamu ili kuweza kuboresha shindano
hilo.
Kigundula
alisema, kwa upande wa Burudani msanii wa kizazi kipya, Tunda Man,
ataongoza safu ya burudani, ambapo itakuwa na wasanii mbalimbali
wakiwemo Dr John, Nabisha kutoka kundi la THT, Fady Dady na wasanii
chipukizi kutoka mkoani hapa.
Kigundula
alisema shindano hilo linatarajiwa kuanza majira ya saa mbili usiku na
kushirikisha warembo 12 ambao watachuana ili kuweza kumpata malkia wa
mkoa huu ambaye atauwakilisha mkoa katika mashindano hayo ngazi ya
kanda.
Warembo
hao ni Hawa Ramadhani (18),Hazina Mbaga (19)Like Abdulraman (19), Irene
Thomas(20), Tatu Athumani (19), Winfrida Gutram (21)Lulu Mbonela (19)
,Hazina Daniel (19),Lulu Matawalo(22),Judithi Moleli (21),Neema Jonas na
Hawa Twaybu(21).
Aliongeza
wa kuwataka wakazi wa Tanga na Mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi
kushuhudia shindano hilo la aina yake, ambalo litajenga historia mypa
kwa Mkoa huu, Shindano la Redds Miss Tanga 2013 limedhaminiwa na
Redds, Miss Tanga, imedhaminiwa na Al Hayat Investment Limited, Dodoma
Wine, CXC Africa,Executive Solutions,Busta General Supply, Mkwabi
Interprises,Lusindic Investment LTD, Lavida Pub,Jambo Leo,Staa
Spoti,Five Brothers Cloud's Media Group, pamoja na Blog Michuzi Media
Group,Bongostaz.com, Saluti5,Kajuna, JaneJohn, na Kidevu na
assengaoscar.blogspot.com.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...