Blog ya Vijimambo ikishirikiana na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Washington, DC, Marekani na Jumuiya ya Watanzania waishio Washington DC, Maryland na Virginia wanapanga kusherehekea miaka 3 ya Vijimambo na kukuletea tamasha la kiswahili. Tamasha hili ni kuendeleza lugha na utamaduni wa Kiswahili hapa Marekani ili watoto wanaoishi huku waweze kuendeleza matumizi ya lugha hii na utamaduni wake kizazi hadi kizazi. 

Siku ya July 6, 2013  hapa DMV kwenye Hall la Hampton Conference Center lililopo 
207 w Hampton Pl, 
Capitol Height, MD

Mambo mengi yatakayokuwepo ni Vikundi mbalimbali vya utamaduni, wanamitindo wa mavazi mbalimbali kuwakilisha, vyakula vya Kitanzania, Wasanii kutoka nyumbani ambao ni Shilole na Masanja Mkandamizaji wakishirikiana na wa hapa Marekani yote hayo ni kudumisha utamaduni wetu wa kiswahili

HOTEL KWA WAGENI 
Tumeongeza vyumba 35 Hotel ya Country Inn & Suites 
Na unapopiga simu uliza SWAHILI CULTURE IN USA kusudi upate unafuu wa bei nambari ya simu ni 301 350 8088 na Address ni
8850 Hampton Malls Drive North
Capitol Heights, MD 20843

Hotel za jirani na hapa ni
Hampton Inn
9421 Largo Dr West,
Largo, MD 20774
simu ni 301 499 4600

Extended Stay American

9401 Largo Drive West,
Largo, MD 20774
simu ni 301 3339139

Confort Inn
56 Hampton Park Blvd
Capitol Heghts, MD20743
Simu ni 301 336 8900

MAVAZI 
10:00 am - 5:00 pm Vazi la Kitanzania
7:00 pm - 3:00 am Vazi lolote lakini uwe umependeza
KARIBU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...