Habari yako ndugu Ankal. 

Mimi ni mwanamke, naandika kwenye blog yako natafuta mchumba, kijana ambaye yupo makini na anayetaka kuanzisha familia hivi karibuni. Awe na umri kuanzia miaka 35 mpaka 39. Naomba sana ambao hawako makini kwenye hili swala wasiniandikie.

Rafiki ninayemtafuta awe hajawahi kuoa, awe hana watoto, awe na elimu kuanzia chuo, awe tayari kupima ukimwi, awe mtu wa kumcha mungu (mkristo), mpole, anayejali na mwenye mapenzi ya dhati.
Napatikana kwenye email address:

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 04, 2013

    Dada mchumba nipo hatuna haja ya kuingia gharama ngoma tunapima kwa macho; vifaa vya mchina noma tupu

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 04, 2013

    Wewe lazima utakuwa kimeo yaani umekosa wanaume mpaka unaamua kutafuta kwenye mtandao, hao wanao kuona kila siku wameshindwa kukutokea kwa ndoa sasa huku kwa ankal ndo itakuwaje??!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 04, 2013

    Hizo sifa zote, bado awe single tu?. Lower your expectations Sister.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 04, 2013

    kabla hatujaingia kwenye usumbufu wa kuandikiana barua hebu weka picha yako tuangalie usafiri wako na jinsi ulivyo kama pia unalingana na jinsi tulivyo maana siku hizi magari sio injini magari ni shape injini hata likikufia mbele ya safari lakini kwa nje mtu hajui kama bovu

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 04, 2013

    Ankal muunganishie na yule jamaa wa Ujerumani aliyekuwa anatafuta mke.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 04, 2013

    unavyoonekana utakua mnoko mnokoooo!halafu unajiskia.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 04, 2013

    Kwa sifa anazotaka inabidi akjifanyie promo kanisani sio humu.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 04, 2013

    Dada umejitahidi kujitosa hapa! Wapo wengi wanaotafuta wachumba na sababu za vigezo vingi na vikubwa kama hivi ndiyo inasababisha kukosa wa kuishi naye.
    Domina usijali hizi ndoa tumekaa huko title tu kujiita mama au baba fulani we kula raha kama mambo yako safi jipatie katotoo hata ka kuadopt. Ule raha. Unajitafutia maradhi ya moyo. Asilimia 50 ya ndoa unazoziaona ni majina tu!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 04, 2013

    wewe dada ni mzima kweli?una shida ya mwenza halafu unaweka masharti kama ya UN?? ndo maana umechina kwa kujidai selective sana.kumbuka mchagua nazi..

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 05, 2013

    Da nimecheka sanaaa kwa kusoma maoni na wala si alichoandika huyu dada.anyway goodluck sister in ur mission to find soul mate.

    ReplyDelete
  11. Kumbe twaweza kufungisha ndoa humu humu, yule jamaa wa miaka 50, alieoa mara mbili, akatapeliwa watoto na mfilipino, sijui mvenezuela anamfaa huyu dada yetu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...