Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishuka kutoka kwenye kivuko cha MV Sengerema tayari kufungua kampeni za udiwani kata ya Nyampulukano.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akisalimia na wakazi wa Sengerema waliokuja kumpokea Busisi leo.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akisalimiana na Hashimu Lundenga,mara baada ya kuwasili Busisi ,Sengerema leo.

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akisalimiana na wakazi wa Sengerema katika viwanja vya shule ya Msingi Sengerema.
 Mzee  Bukilo akiongoza kundi lake wakati wa mkutano wa hadhara wa ufunguzi wa kampeni kata ya Nyampulukano, wilaya ya Sengerema ,Mwanza.
 Mbunge wa Sengerema ,William Ngeleja akihutubia wakazi wa kata yaNyampulukano na kuelezea jinsi ilani ya uchaguzi ilivyotekelezwa pamoja na ufafanuzi juu ya mradi mkubwa wa maji kwa wakazi wa Sengerema.
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita, Ndugu Joseph  Kasheku  'Musukuma' akihutubia wakazi wa Sengerema wakati wa ufunguzi wa kampeni za udiwani kata Nyampulukano,Sengerema, Mwanza.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Taifa, Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Nyampulukano, Sengerema wakati wa ufunguzi wa kampeni za udiwani. Juni, 3, 2013.
Mgombea kiti cha udiwani kata ya Nyampulukano  kupitia CCM,Ndugu Charles Gabriel Rugabandana akisalimia wananchi mara tu baada ya kutambulishwa rasmi.Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika tarehe 16,Juni,2013. Picha na Adam H. Mzee

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 04, 2013

    Nape fanya mazoezi. tumbo limeshaanza kukua!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 04, 2013

    Katiba Mpya MAWAZIRI WANASIASA OUT!
    mnapendeza hukohuko kwenye kelele na uongo nchi inataka Mtu Kazi!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 04, 2013

    Hivi watu kila siku kukusanyika katika mikutano ya siasa wanapata muda gani wa kufanya kazi za kuendeleza maisha yao? kila kukicha tunaona halaiki ya watu wakihudhuria mikutano hii, laiti wangelikuwa wanatumia muda na juhudi hizi katika kuinua kiwango chao cha maisha!!!!!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 04, 2013

    na wewe "kila kukicha tunaona halaiki ya watu wakihudhuria mikutano hii."

    Na wewe kila kukicha uko online!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...