Mfuko wa pensheni wa PPF unapenda kuwakaribisha wadau wote kutembelea katika banda la PPF kwenye maonyesho ya kimataifa ya biashara ili kuweza kujua shughuli mbalimbali zinazofanywa na mfuko wa pensheni wa PPF kama vile Taarifa za michango, Usajili, mafao , uwekezaji ikiwemo mikopo ya SACCOS kwa wanachama wa PPF.
Afisa wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. Juma Mwita akitoa maelezo kuhusu michango kwa mwanachama wa PPF, mara baada ya kumkabidhi taarifa ya michango yake katika banda la PPF kwenye maonyesho ya kimataifa ya biashara yanayoendelea kwenye viwanja vya mwalimu JK Nyerere jijini Dar es Salaam.
Afisa wa Idara ya Mifumo ya Habari wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi. Hawa Kimaro akitoa maelezo kuhusu michango kwa mwanachama wa PPF, Bw. Walter Vasolela mara baada ya kumkabidhi taarifa ya michango yake katika banda la PPF kwenye maonyesho ya kimataifa ya biashara yanayoendelea kwenye viwanja vya mwalimu JK Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mdau wa PPF akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mwandamizi wa kanda ya kusini ya PPF, Bw. Thomas Chisanga alipotembelea banda la PPF.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. bwana michuzi naomba nipitishie salamu zangu kwa kupitia blog yako kwa ndugu yangu thom chisanga nikimpa hongera kwa kuchapa mzigo nampa hongera sana kwa mafanikio yake.

    mimi nduguyo hamisi wa m-nyamala.
    nikiwa masomoni USA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...