KINYANG’ANYIRO cha kumpata Redd’s Miss Tanzania kwa mwaka huu kinazidi kushika kasi na sasa, kazi kubwa ipo katika ngazi ya kanda, pale kutakapokuwa na kazi ya kumsaka mrembo wao ndani ya wiki hii.

Kazi kubwa itakuwa katika kumpata Redd’s Miss Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Redd’s Miss Kanda ya Mashariki na Redd’s Miss Kanda ya Ziwa.

Shughuli itaanza kesho, wakati warembo zaidi ya kumi watakapopanda jukwaani katika Ukumbi wa Mikutano wa Mtende, uliopo Soweto Mbeya, kumsaka Redd’s Miss Nyanda za Juu Kusini.

Katika shindano hilo linalotarajiwa kuanza saa 2 usiku, burudani kali inatarajiwa kutolewa na bendi ya FM Academia, huku kiingilio kikiwa ni Sh 10,000 kwa viti vya kawaida na Sh 25,000 kwa viti maalumu.

Keshokutwa itakuwa kazi pevu kwa warembo wa Redd’s Miss Kanda ya Mashariki, ambao watapanda jukwaani katika hoteli ya Nashera mjini Morogoro, kumsaka yule atakayefanikiwa kutwaa taji.

Wanne Star pamoja na wasanii wengine wa Morogoro ndio watakaonogesha shindano hilo, ambalo kiingilio chake kitakuwa Sh 10,000 kwa viti vya kawaida na Sh 20,000 viti maalumu.

Siku hiyo pia atasakwa Redd’s Miss Kanda ya Ziwa, shindano ambalo litafanyika katika ukumbi wa Nyerere ndani ya hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza.

Pia kutakuwa na burudani za kumwaga zitakazoongozwa na mkali wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz akishirikiana na Michael Ross na kiingilio kitakuwa Sh 20,000 viti vya kawaida na Sh 40,000 viti maalumu.

Shindano la Redd’s Miss Tanzania kwa sasa linadhaminiwa na kinywaji cha Redd’s Original kinachozalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...