MKURUGENZI WA KADI'S INVESTIMENT LTD ANAWATANGAZIA WANANCHI WOTE KUWA ANAUZA SHULE YAKE YA KADI'S ENGLISH MEDIUM PRIMARY SCHOOL ILIYOPO WILAYANI BUKOMBE MKOANI GEITA. 

SHULE INAENEO LA HEKA KUMI LILOSAJILIWA KWA NAMBA 20588 L.O NAMBA 186857. INAVYUMBA VYA MADARASA KUMI OFISI YA UTAWALA NA YA WATUMISHI. KUNA BWENI LA KULAZA WANAFUNZI 150 AMBALO HALIJAKAMILIKA NA KUNA VIWANJA VYA MICHENZO.

SHULE IMESAJILIWA KWA NAMBA SH.07/7/E.A001 TAREHE 2.12.2004 KWA SHULE YA AWALI NA NAMBA SH.07/7/001 KWA SHULE YA MSINGI. 

KWA MAWASILIANO PIGA NAMBA 0713922890 na 0789499563.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 21, 2013

    Ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni!!!

    Kwa herufi kuuubwa tna bila wasi wasi Bango la tangazo linasomeka ''SHULE INAUZWA'' !

    Haya usingeyaona Kipindi cha baba wa Taifa Kambarage ungesikia kitu kama hiki huyo muhusika kama hakwenda Gerezani atapelekwa Hospitali ya Vichaa.

    Hii yote ni kutokana na kuingia ktk Mfumo wa Ubepari ambapo kila kitu ni rasilimali!, na kila kitu ni gharama!

    Pana aliekuwa kipindi hicho aliekuja kujua kuwa Maji ya kunywa itakuwa biashara?, watu walijua ya kuwa Huduma za Choo cha kujisaidia ama Bafu la kuogea pia ni Biashara?

    Huko tuendako tusije kushangaa kusikia SHIRIKA LANGU LA UMEME LA TANESCO NILILINUNUA NA SASA NALIUZA!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 21, 2013

    Kwa mara ya kwanza nasikia mtu anauza shule. Ama kweli, Kimfaacho mtu chake.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 21, 2013

    Sasa mbona ukutani imeandikwa Kadi's Secondary school hali wewe unasema shule yako unayoiza ni ya awali na msingi? Au picha hizo siyo za shule unayouza?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 21, 2013

    kaka michuzi sijaelewa,tangazi limesema shule ya english medium inauzwa,ni pamoja na walimu,wafanyakazi wanafunzi na majengo au ni majengo tu (pamoja na ardhi bila shaka ) kama ni majengo na ardhi basi hiyo ya english au kiwsahili medium si muhimu.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 21, 2013

    Mjomba Michuzi !

    Shule inauzwa?

    Kwa mwendo wako na Wadau wako hatutashangaa siku moja ukitangaza na kuweka Namba za simu za Muuzaji kwa vitu kama:

    1.KOFIA YA POLISI KUUZWA!!!
    2.MAHAKAMA YA MWANZO KUUZWA!!!
    3.HOSPITALI KUUZWA!!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 21, 2013

    Katika vitu vilivyotuathiri sana nchini na kutugharimu sana ni TRANSFORMATION from SOCIALISM to CAPITALISM!

    Hapa ni ule mtazamo imeruhisiwa mtu binafsi kumiliki shule, sawa na je kuuza shule kiholela imeruhusiwa?

    Huwezi kusikia nchi kama Sweden, Norway, Canada ama Japan Shule ikiuzwa, hii ni made in Tanzania peke yake.

    Hivi jamani, Serikali na kuanguka kwa Kiwango cha Elimu nchini bado hakuna Sera zinazo zingatia Umuliki wa Taasisi za Elimu kama shule?

    Inafikia mtu analala usingizi anazinduka anapata mawazo mapya anaamua kuiuza shule wakati Elimu inayotolewa ktk shule ni mali ya umma ingawa shule inamilikiwa na mtu binafsi sio hoja sana lakini huwezi kuiuza shule kiholela kama unauza Banda la Mbuzi au Kuku.

    Kwa sababu kinachotolewa shuleni yaani Elimu ni mali ya Mamlaka ama Umma.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 21, 2013

    kweli bongo sasa tuko kibiashara, yaani ni mara yangu ya kwanza kusikia shule inauzwa hahahaha, ts fun though..

    sasa vipi kuhusu walimu na wanafunzi??nao wako inclusive kwenye kuuzwa??au ni majengo tu ya shule na sio shule??

    hahahaha kiswahili nacho mhhhhh...

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 21, 2013

    Ohhh Mjomba Michuzi!

    Yaani na wewe umekuwa na moyo wa kibepari namna hii?,,, hata siamini.

    Wewe na Mabepari wako uzeni kila kitu lakini mtuachie vitu hivi hapa chini:

    1.Serikali yetu na Raisi wetu mpendwa Mhe. Dr.Jakaya Kikwete.

    2.Klabu za Yanga na Simba.

    3.Chama cha Mapinduzi.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 21, 2013

    Hahhh!

    tutakuja kisikia Msikiti ama Kanisa linauzwa!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 21, 2013

    Du!!!! hii kweli kali m2 anauza shule itafikia kipindi ss watu watakuja kuuza hospitali hiyo ndo bongo bwana mungu ibakiri TZ na watu wake..

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 21, 2013

    Maisha yabadilika, sijui kama ni progress ama ni janga la capitalism.Ewe bwana miye nitangazie, nauza mguu wa shoto

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 22, 2013

    Nimecheka mpaka nikaenda Hospitali/Emergecy, loooo!!!

    Jamani jamani msimug'oe macho Michuzi, Michuzi ni mjumbe tu.

    Ama kweli mahoka.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 22, 2013

    Acheni longo longo nyingi mnashangaa nini sasa? Michuzi hebu mwambie aweke bei wenye pesa tuangalie kama inalipa..!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 22, 2013

    Ohhh!

    Hii kasi ya maisha ni balaa, hadi Shule inauzwa?


    Ama kweli UJAMAA NI UTU na UBEPARI NI UNYAMA!

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 22, 2013

    Naungana na Mdau wa 6 hapo juu TRANSFORMATION from SOCIALIMS TO CAPITALISM.

    Kwa kuwa wastani wa Shule na Viwango kukidhi mahitaji yetu ya kuelimisha bado haujakaa ktk uwiano sio suala la busara mtu akauza Shule kiholela.

    Mamlaka na Umma unahitaji zaidi uelimishaji ambao unafanyika ktk Shule licha ya kuwa mmiliki anaweza kuwa mtu binafsi.

    INAELEWEKA MUUZAJI NI LAZIMA ATAZIELEKEZA FEDHA ATAKAZO VUNA KWA MAUZO KWENYE SEKTA ZINAZOKUBALIKA KAMA KILIMO AMA MADINI.

    ISIPOKUWA LA MUHIMU ANGEWEKA WAZI MNUNUZI ATAENDELEA KUYAFANYA MAJENGO NA MADARASA KUWA SHULE AMA AMEPATA MAWAZO MAPYA YA KUFUNGUA BAA AMA KILABU CHA POMBE ZA KIENYEJI NA GESTI?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...