Madini ya vito aina ya Tanzanite yanayopatikana na kuchimbwa Tanzania pekee duniani hapa yamekuwa kivutio kwa wananchi katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma-Afrika yanayoaendelea jijini Accra-Ghana. 
Wananchi wengi waliotembelea banda la Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) wameeleza kuwa pamoja na kuyaona madini hayo sehemu mbalimbali duniani lakini walikuwa hawana ufahamu wa kutosha kuwa ni Tanzania pekee ndiyo yenye hazina ya madini hayo. 
Msemaji wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) Eng. Yisambi E.Shiwa ameeleza kuwa maonesho yamekuwa yakitumika kama nyenzo ya kutoa elimu kuhusu uendelezaji wa sekta ya madini Tanzania ili kuweza kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya Tanzania kuwekeza kwenye rasimali hiyo.
Kamishina wa Tume ya Utumishi wa Umma Ghana Bw.Robertson Akwei Allotey akiangalia madini ya tanzanite yanayoonyeshwa katika banda la Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) jijini Accra
Wananchi wa Ghana wakiwa kwenye banda la Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) ili kupata elimu kuhusu sekta ya madini Tanzania jijini Accra

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 22, 2013

    TANZANIA NI NYUNDO YA CHUMA!

    Watake wasitake tunawaburuza, Mhe. Raisi Kikwete habari ndio hizo, tunahitaji kurekebisha mapungufu yatu ili TUENDELEE KUTESA KTK KILA IDARA!

    Kama unavyoona Vijana wako wakitesa huko Ghana, huku Dunia nzima ikija Tanzania ktk Ujumbe wa Mgeni na ukijiandaa kuupokea mwishoni mwa mwezi huu Mgeni BROTHER BIG BARRACK atakapoingia !

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 22, 2013

    Mdau wa kwanza Nakupa 5 !

    TANZANIA ZAIDI YA KUWA NYUNDO YA CHUMA, tuseme '''TANZANIA NI NYUNDO KUBWA'''! AMBAYO HATA KAMA UKIRUSHIWA UKIJIFANYA KUI PANCHI UMESURURIKA UTAVUNJIKA SHINGO AMA KICHWA KAMA HUKU FARIKI KABISAAA.

    WAPINZANI WWETU WAKUBWA NA HASA NDUGU ZETU WAKENYA WAMEKUWA NA KAMPENI CHAFU SANA KUTUHUJUMU LAKINI SASA IMEFIKIA MWISHO AROBAINI YAO IMETIMIA, TIUMESHAA ANZA KUWABURUZA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...