wajumbe wakifutili a mada
Meneja wa Kanda ya Mshariki na Kusini wa TFDA, Bw. Emanuel Aphonce, akiwasilis ha Mada kwa wajumbe.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bw. Hery Nkunda, akitoa maelezo ya utangulizi katika mkutano huo.
Mgeni rasmi, Dkt. Saiduma Kaduma akifungua mkutano wa Wakaguzi wa TFDA
======== ===== ========
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imekutana na wakaguzi wa bidhaa za Chakula, Dawa, Vipodozi na vifaa tiba wa kutoka mikoa ya Mtwara na Lindi kwa lengo la kukumbushana maadili na kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili katika udhibiti ususan ukaguzi.
Mkutano huo wa siku mbili unafanyika mkoani Mtwara kwa tarehe 4 na 5 Juni, 2013, umefunguliwa rasmi na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Dkt. Saiduna Kabuma.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bw. Hery Nkunda, katika maelezo yake yaUtangulizi alisema kuwa mkutano huo unalenga kukutana na wakaguzi wa TFDA katika Halmashauri walau mara moja kwa mwaka ili kubaini changamoto za ukaguzi, kujadili na kukubaliana mikakati endelevu katika ukaguzi wa bidhaa za chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba nchini.
Akihutubia washiriki wa mkutano huo kabla ya kufungua rasmi mgeni rasmi, dkt. Kabuma amewataka wakaguzi kutumia Sheria, kanuni, maadili, hekima na busara katika kufanya kazi za ukaguzi. Aidha aliwataka wakaguzi kutoka ofisini na kwenda nje kuangalia yanayofanyika kama ni kwa mujibu wa Sheria au la.
TFDA imekasimu baadhi ya majukumu ikiwa ni pamoja na ukaguzi wa bidhaa kwa Halmashauri. katika kuboresha hili, TFDA imekuwa na utaratibu wa kukutana na wakaguzi walio katika Halmashauri Mbalimbali nchini kwa lengo la kubadilishana mawazo na kujadili mikakati ya udhibiti.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...