Uchaguzi wa viongozi wa BFT uliopangwa Kufanyika tarehe 7/7/2013 jijini
Mwanza, utafanyika kwa tarehe hiyo kama ulivyopangwa.
Kikao cha kamati ya utendaji ya BFT kilichofanyika juzi katika ofisi za
BFT kikiongozwa na Rais wa shirikisho Joan Minja kimesisitiza kuwa
uchaguzi utafanyika kama ulivyopangwa na haujaairishwa kama baadhi ya
kikundi cha watu wachache wanaojiita wadau wanavyoweka pingamizi na
kupotosha kwa kuwashawishi wajumbe wa mkutanao mkuu hasa kutoka
mikoani kutohudhuria mkutano huo wa uchaguzi,kwa manufaa yao binafsi
na kinyume na katiba yetu.
Upotoshaji huo unafanywa na Akaroly Godfrey aliyekuwa kiongozi katika
uongozi uliojiudhuru kutokana na kashfa za kusafirisha madawa ya kulevya
na kusababisha Tanzania kufutwa uanachama na chama cha ngumi cha
dunia (AIBA) na kusababisha kutoshiriki mashindano,mikutano na shughuri
zote za kimataifa za chama cha ngumi cha Dunia AIBA. Naomba wadau
na serikali kuwa makini na watu wanaoshawishi kwa lengo la masilahi yao
binafsi na kusababisha michezo kudolola badala ya kusonga mbele.
Fomu za uchaguzi zilishaanza kutolewa na Baraza la Michezo la Taifa
(BMT) toka tarehe 4//2013 na zitaendelea kutolewa hadi tarehe 4/7/2013
jijini Mwanza na tarehe hiyo ndio itakuwa siku ya mwisho ya kuchukua na
kurudisha fomu, tarehe 5/7/2013 itatakuwa siku ya usaili na utafanyika jijini
mwanza, tarehe 6/7/2013 kupitia pingamizi na kuzitolea maamuzi na tarehe
7/7/2013 ndio siku ya uchaguzi.
Kimsingi taratibu zote za kuitisha uchaguzi kwa mujibu wa katiba yetu
zimezingatiwa na zimekamilika.
Aidha BFT inatoa tamko kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu kufika katika
uchaguzi uchaguzi, ili kupata viongozi halali kwa mujibu wa katiba,
waendelee na shughuri za kuendeleza mchezo wa ndondi na kuaandaa timu
ya taifa kushiriki katika mashindano ya Afrika nchini Mauritius Sept. 2013
BFT inatoa wito kwa watu wote wenye sifa, nia, moyo na uwezo wa
kuongoza wajitokeze kuchukua fomu za kugombea uongozi kwani wakati
ndio huu.
Makore Mashaga
Katibu Mkuu.


.bmp)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...