Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani , ( wapili kutoka kulia) akiongozwa na Meya wa Mansipaa ya Morogoro, Amiri Nondo ( watatu kulia ) , kwenda kukagua baadhi ya mabanda ya Halmashauri mbalimbali nchini katika uwanja wa Jamhuri wa Mjini Morogoro na ( wa kwanza kulia) ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Amanzi , ni baada ya kufungua maadhimisho ya wiki ya Serikali za Mitaa kitaifa , Juni 24, mwaka huu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani , ( kulia) akionesha ishara ya kusalimia wanafunzi wenye ulemavu wa kiziwi kutoka shule ya msingi Kilakala , Manispaa ya Morogoro , katika banda la Halmashauri hiyo , baada ya ufunguzi wa maadhimisho ya siku za Serikali za Mitaa nchini zilizoanza Juni 24, mwaka huu na kufikia kilele Julai mosi mwaka huu ( wapili) ni Meya wa Manispaa ya Morogoro , Amiri Nondo.
Ufugaji nyuki , banda la Shirika la Elimu Kibaha, , Idara ya Maendeleo ya Jamii.
Baadhi ya viongozi wa Halmashauri za Wilaya mbalimbali nchini wakimsikiliza mgeni rasmi , Waziri wa Utumishi, Celina Kombani ( hayupo pichani) siku ya ufunguzi wa wiki ya Serikali za Mitaa , Juni 24, 2013.
Bendera za aina mbalimbali zikiwa zinapepea katika uwanja wa Jamhuri wa Mjini Morogoro kuashiria ushiriki wa Halmashauri za Wilaya kwenye maonesho ya maadhimisho ya wiki ya Serikali za Mitaa Kitaifa.
Baaadhi ya wananchi wakisikiliza maelezo ya mtaalamu wa mradi wa mabasi yaendayo haraka (DART) unaolenga kuondoa msongamano wa magari kati kati ya Jiji la Dar es Salaam.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...