Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeupongeza Uongozi wa Benki ya Kiarabu kwa Maendeleo ya Afrika (BADEA) kwa hatua zake kubwa ilizoonyesha katika kusaidia maendeleo ya Kiuchumi na kijamii hapa Zanzibar.
Pongezi hizo zimetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika hafla fupi ya uzinduzi wa ujenzi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar { SUZA } awamu ya kwanza uliopata ufadhili mkubwa kutoka kwa Benki hiyo ya Badea hapo Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.
Pongezi hizo zimetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika hafla fupi ya uzinduzi wa ujenzi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar { SUZA } awamu ya kwanza uliopata ufadhili mkubwa kutoka kwa Benki hiyo ya Badea hapo Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.
Baloz Seif ambae alimuwakilisha Rais wa Zanzibar kwenye uzinduzi huo alisema Benki ya Maendeleo ya Kiislamu { BADEA } imekuwa mshirika mkubwa wamaendeleo wa Zanzibar hasa katika sekta ya Elimu hatua ambayo inaijengea mazingira ya mfumo mzuri wa miundo mbinu ya Kielimu hapa Zanzibar.
Alisema sekta ya Elimu ni moja kati ya mambo yaliyopewa msukumo mkubwa ndani ya dira ya maendeleo ya Zanzibar ya 2020 katika muelekeo wa kuwajengea uwezo wa Kielimu vijana wanapomaliza masomo yao wakubalike kuingia moja kwa moja katika soko la ajira.
“ Chuo chetu Kikuu cha Taifa cha Zanzibar { SUZA } tunakusudia kukijengea uwezo mkubwa zaidi utakaowapa fursa pana wanafunzi wetu kuingia katika soko la ajira sio Tanzania na Afrika Mashariki bali popote pale Duniani “. Alifafanua BaloziSeif.
Balozi Seif alisisitiza kwamba licha ya ongezeko kubwa la idadi ya watu liliopo hivi sasa Nchini lakini bado Serikali imejikita kuongeza Skuli zaidi nyengine za Sekondari Unguja na Pemba kwa kushirikiana na wadau wa sekta hiyo ili kuwajengea mazingira bora wanafunzi yatakayowawezesha kupata fursa ya uhakika ya kujiunga na vyuo vya Elimu ya juu.
Akitoa salamu za Benki ya Maendeleo ya Kiislamu { BADEA } Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo Mhandisi Youser Ibrahim Albassam alisema ujenzI wa vyuo Vikuu ni moja ya hatua nzuri kwa Taifa lolote katika kuelekea kwenye maendeleo ya uhakika.
Mhandisi Albassam ambe pia ni Makamu Mwenyekiti na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Saudi Arabia alisema Benki hiyo itaendelea kuunga mkono juhudi za maendeleo za Zanzibar.
Alisema kupitia Bodi ya Wakurugenzi wa Benki Hiyo Mhandisi Albassam alieleza kwamba Uongozi wa Benki hiyo umeahidi kusaidia tena Dola za Kimarekani Milioni kumi { U$ Dolla 10,000,000 } kwa ajili ya kuendeleza awamu ya pili ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar { SUZA } katika Kampasi yaTunguu.
“ Tumefarajika na ukarimu wa watu wa Zanzibar na mazingira yake mazuri yaliyopelekea kuushawishi Uongozi wa Benki yetu ya Badea kusaidia Sekta ya Elimu, Bara bara na Nyanja nyengine za maendeleo “. Alisisitiza Mwenyekiti huyo wa Bodi ya Wakurugenzi ya Badea Mhandisi Albassam.
Mapema Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar { SUSA } Profesa Idriss Rai alisema ujenzi huo umeongeza program nyengine na kufikia nane kutoka Nne kutokana na mabadiliko ya mahitaji Kiuchumi sambamba na Kijamii hapa Nchini.
Profesa Rai alizitaja baadhi ya program hizo kuwa ni pamoja na masomo ya Sayansi ya mazingira ,Biashara, Utalii na Kilimo pamoja na kuanzishwa kwa vituo viwili vya utafiti vya mazingira na Kiswahili.
Makamu Mkuu huyo wa Suza alifahamisha kwamba muelekeo wabadae wa chuo hicho kikuu cha Taifa cha Zanzibar ni kukiwezesha kuhudumia wanafunzi kutoka kanda ya Afrika Mashariki na maeneo mengine ya mbali.
Alieleza kuwa hatua hiyo imekuja kufuatia Zanzibar kubarikiwa kuwa na bahati ya kupokea wanafunzi wengi kutoka sehemu mbali mbali nje ya Tanzania kwa ajili ya kujakujifunza hasa masuala ya lugha.
“ Tutalazimika kujikita pia katika kuwajengea mazingira bora ya makazi wanafunzi wetu hasa wale wa kigeni na hili linahitaji pia kuungwa mkono na wadau wetu wa elimu “. Alieleza Profesa Rai.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimpatia zawadi ya mlango Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Kiarabu kwa Maendeleo ya Afrika (BADEA) Mhandisi Youser Ibrahim Albassam kama ishara ya uongozi wa Benki hiyo kukaribishwa rasmi Zanzibar. Zawadi hiyo alimpatia katika hafla fupi ya uzinduzi waujenzi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar { SUZA } kampasi ya Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.
Balozi Seif akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi BADEA Mhandisi Youser Ibrahim Albassam mara baada ya uzinduzi waujenzi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar { SUZA } kampasi ya Tunguu.Pembeni yao ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ali Juma Shamuhuna.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Sei akizungumza na Ujumbe wa BADEA ulioongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo Mhandishi Yousef Ibrahim Albassam hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiagana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya BADEA Mhandishi Yousef Ibrahim Albassam pamoja na ujumbe aliofuatana nao mara baada ya mazungumzo yao.
Ujumbe wa BADEA ulikuwepo Zanzibar kuhudhuria uzinduzi wa ujenzi wa chuo kikuu cha Taifa cha Zanzibar { suza } katika kampasi ya Tunguu.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
Michuzi blogu ya jamii ifahamishe wadau kwa kina kuwa benki ya BADEA jina lake rasmi ni The Arab Bank for Economic Development in Africa na tovuti yake ni www.badea.org na madhumuni yake ni is a financial institution funded by the Governments of the Member States of the League of Arab States on 18 February 1974.
ReplyDelete[1] It is an independent international institution enjoying international legal status and autonomy in administrative and financial matters.
Its headquarters is located in Khartoum, the capital of the Republic of Sudan.
BADEA was created for the purpose of strengthening economic, financial and technical cooperation between the Arabia and Africa and for the embodiment of Arab-African solidarity on foundations of equality and friendship.
To achieve this, the Bank was given a mandate to:
Participate in financing economic development in African countries;
Stimulate the contribution of Arab capital to African development;
Help provide the technical assistance required for the development of Africa.
The projects financed by the Bank are priority projects of the beneficiary countries and usually form part of their development plans.
In some instances, these projects are of a regional character benefiting several countries simultaneously and helping in their economic integration.
BADEA also provides technical assistance in the form of non-refundable grants.
Mdau
Jijini Khartoum, Sudan.
Taarifa ina upungufu, BADEA ni Benki ya Kiarabu kwa Maendeleo ya Afrika na sio Benki ya Maendeleo ya Kiislamu. Acronym BADEA urefu wake ni Arab Bank for African Development. Waandishi muwe makini na kazi zenu.
ReplyDelete