ANKAL

NAOMBA UUFIKISHE UJUMBE HUU KWA WAHUSIKA WAWEZE KUTUSAIDIA KUONDOA KERO HII. 

HUYU BWANA YUPO MATAA YA UBUNGO KAMA TULIVYO MNASA LEO ASUBUHI, ANAKAWAIDA YA KUJA KUSAFISHA KIOO CHA GARI NA MARA NYINGI HUPANDA KWENYE BONAT YA GARI KUKAA NA KUEGEMEA KIOO KAMA HUTO MPATIA SENTI KIDOGO YA HUDUMA ALIYOTOA BILA KUTUMWA.

 AMEKUWA NI KERO SANA KATIKA ENEO HILO. TUNAOMBA WAHUSIKAWATUSAIDIE KUONDOA KERO HII PAMOJA NA WENGINE WALIOZAGAA MAENEO YOTE YA MATAA HAPA MJINI.

 AHSANTE SANA
 MDAU.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 04, 2013

    kwakweli hii kero naomba serikali ingeingilia kati, we are being terrorised in our own cars, yani nikifika kwenye mataa yoyote naanza kuhaha manake najua tu wataniattack. this is really irritating. serikali iingilie kati tafadhali.
    mdau

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 04, 2013

    Jamani, huyu jamaa ni mkorofi na mbabe sana . alikuwa tazara, akahamia foleni ya buguruni na sasa yupo ubungo. Tabi ahii anapenda zaidi kuifanya katika magari wanayoendesha wadada au wamama. Mimi alishawahi mara mbili kupanda katika gari yangu. mara ya pili, nilipokauka kumpa pesa, aliamua kuvunja wiper moja ya gari , nilipomtishia kumgonga akaondoka, ila alishaivunja moja duh . Tafadhali naomba wahusika wasaidie kushughulikia hili jambo. mdau aliyeleta hii picha namshukuru.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 04, 2013

    Huyo jamaa yupo tena anatishia usalama kwa ambaye umeshindwa kumlipa ujira kwa kazi ambayo hakupewa,hivyo tunaomba wahusika wamuondoe pamoja na wengine wanaofanya kazi kama yake humo barabarani.Chonde chonde tusaidieni kuondoa kero hii ya waosha vioo barabarani.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 04, 2013

    waacheni wapige hela, ajira hakuna. kwanza huyo mjuba mkimtoa hapo atarudi kutupiga roba sisi walala hoi maana alikuwa anapiga roba za mbao maeneo ya kigogo njiapanda pale, sasa tumepumzika nanyie wenyemagari mumuwezeshe hata hamsini tu sio mbaya hakatai nauhakika.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 04, 2013

    Morroco pia! mie nilishaenda mbaka pale oysterbay polisi kutoa repoti so far no change. Authorities mko wapi? its unfair that we are being terrorised by a handful of people. THIS THING HAS TO STOP!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 04, 2013

    kesho mtasikia amegongwa, subirini, namlia timing. Watu kama hao hatuwahitaji duniani.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 04, 2013

    Yaani wote ninyi waoga wa kupitiliza, mtu mmoja anwashinda, si ushuke to umzabe vibao kama analeta upuuzi,nitamlimba mpaka atoe kamasi.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 04, 2013

    huyu mie nilishuka nikatanua kifua na kofi juu akasepa

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 04, 2013

    Huyo ni mhalifu kama wengine ni sawa na kibaka anayekwapua na kukimbia. Inabidi askari wamchukue kwa hatua za kisheria.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 04, 2013

    Kama kawaida mpa janga litokee ndipo wahusika watachukua hatua muafaka!!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 04, 2013

    Polisi wanasema raia tushirikiane nao katika kufichua uhalifu na viashiria vyake? Sasa nini tatizo katika kupambana na janga hili ambalo tumetumia njia mbalimbali kuwajulisha polisi?










    /

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 04, 2013

    Jamani, Kamanda Kova si keshatangaza kuwa hawa ni wahalifu?

    Nini kinasubiriwa?

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 04, 2013

    ni vile bongo magari yanakua mengi kwenye foleni, vinginevyo, unamuacha apande kwenye bonet halafu unaendesha gari na kufunga break ya ghafla, tupa kuleeee..Kero yote kwishneyyyy...

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 04, 2013

    Nimekubali na kauli ya wenzangu hapo juu.. sio vizuri kumlazimisha mtu yeyote kusafisha vioo wakati hajatumwa... lakini kuna vijana wadogo hata maeneo ya Tabata, Pugu road Nk. Ambaye watakusafishia express kabla ya taa kijani kuwaka... nachosifu ni yupo juani kupata kitu chochote ambyae ni mara miya bora kuliko kuomba au kukunyanganya au kutoa madhara ya aina yeyote... pia swala hili lifikiriwe nchi yetu ajira inakuwa ngumu zaidi... au wachambueni wapele maeneo ya kuocha magari..

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 05, 2013

    Hawa jamaa wasumbufu sana. Mimi yalishanikuta pale mataa ya morocco, jamaa kaja kaanza kusafisha kioo wakati gari langu ndio kwanza nimetoka kulichukua baada ya kulisafisha pale sheli ya victoria. jamaa kavania kioo na kuanza kupaka mapovu. nilipomwambia aache akapandisha waiper na kupaka mapovu mengi wakatihuo taa zilisharuhusu magari lakini nikashindwa kuondoka kwani sioni mbele. ile nashuka kurudisha waiper naona wenzake wawili wanafungua milango ya gari wanataka kuchukua pochi yangu. kwakweli inakera sana na ikitokea umeacha kioo wazi wanakwapua chochote kilicho karibu. tunaomba wahusika walushughulikie hili tatizo kabla majanga makubwa hayajatokea
    TML

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 05, 2013

    Hawa watu wapo wengi kwene hizi taa za barabarani na wanaleta kero kubwa. Juzi nilipita moroko tena nimetoka kuosha gari pale Victoria lakini cha ajabu bado alikuja kijana kunioshea kioo .. pamoja na kuwasha wiper blades bado akazinyanyua na kusafisha then he asked for money. Kumnyima ikawa kosa mana yale maji kwene kopo lake akamwagia gari Zima na kuanza kutukana huku akigonga gari. Kama vioo vingekua wazi sijui angenifanya nini. Inaogopesha kwakweli

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...