
DPP anapoona hana mashahidi thabiti wa kuja kujenga kesi yake anatumia kifungu hicho kufuta kesi kwani kuendelea kuwa na kesi za jinai mahakamani ambazo anaona kabisa hana mashahidi thabiti wa kuwaleta mahakamani ni matumizi mabaya ya sheria na kuisababishia Serikali gharama pamoja na mrundikano wa kesi mahakamani kwa ajili ya kuanza kusikilizwa lakini Wakili wa Serikali, Awamu Mbangwa aliwasilisha hati hiyo, chini ya Kifungu cha 91 (1) cha Mashauri ya Jinai (CPA), kwa niaba ya DPP akiomba kesi hiyo ifutwe kwa sababu hana nia ya kuendelea kuwashtaki washtakiwa hao.
Baada ya kuwasilisha hati hiyo.
Hakimu Mugeta alikubaliana na ombi hilo na kuifuta. Mmoja wa mawakili wanaowatetea washtakiwa hao, Alex Mgongolwa alisema hawana pingamizi la kufutwa kwa shauri hilo ingawa walitaka waelezwe sababu za hatua hiyo.
Mgongolwa alisema walitaka kujua sababu hizo kwani walikuwa na wasiwasi kuwa wateja wao wangeachiwa huru na kukamatwa tena baada ya muda mfupi na kupandishwa kizimbani. Kutokana na shaka hiyo, waliiomba Mahakama kuwapa kinga.
Akiifuta kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 3/2013 na kuwaachia huru washtakiwa hao ambao ni Simba na wenzake, Salum Mwaking’inda na Meneja wa Shirika hilo, Victor Milanzi, Hakimu Mugeta alisema maombi ya upande wa mashtaka yamekubaliwa.
Akizungumzia uamuzi huo wa DPP wa kuwafutia kesi wateja wake, nje ya viwanja vya mahakama hiyo, Wakili Mgongolwa alipongeza uamuzi huo akisema ni matumizi ya sheria.
Tanzania wanafungwa wezi wa kuku na simu za mikononi Mafisadi wanaofilisi Makampuni na Taasisi za Umma hawana makosa wao wanfutiwa Kesi na Kufungwa vifungo vifupi!
ReplyDeleteIba wewe kuku uone?
Bongo tAMBARALe ,Tanzania jAMBAland ndio kama tuijuavyo!!!