Katika kuendeleza na kuimarisha mahusiano mazuri kati ya Benki ya NMB na waheshimiwa wabunge, Benki ya NMB iliandaa mtanange wa kukata na shoka ambao ulihudhuriwa na washabiki wa timu hizo mbili ambao ni wakazi wa manispaa ya Dodoma.

Hiki ndicho kikosi kamili cha timu ya benki ya NMB kilichong’ara siku hiyo katika kutimua kivumbi kwenye uwanja wa jamhuri.

Na hii ndio timu ya waheshimia wabunge iliyowatikisa wachezaji wa timu ya NMB

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Mhe. George Mkuchika ambae alikua ndiye mgeni rasmi akikagua kikosi cha timu ya NMB kabla ya mpambano huo.

Naibu waziri wa habari Vijana,Utamaduni na Michezo Mhe.Amos Makalla (Jezi ya njano na Bluu) akipigwa chenga na Afisa mkuu wa fedha NMB Waziri Waziri katika mtanange huo uliokuwa wa kukata na shoka.

Mbunge wa jimbo la Kinondoni Mhe.Iddi Azan ambae ndiye mlinda mlango wa timu ya wabunge (Jezi ya rangi ya chungwa) akiongoza wanatimu kufurahia goli moja walilolipata kwa taabun sana na kuwapa ushindi wa bahati dhidi ya timu ya NMB

Hawa ni sehemu ya mashabiki wa timu hizi mbili wakifurahia mtanange huu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 21, 2013

    aah Josephine Kulwa nakuona!! woman with brain na mchapakazi sana. Hongea mamea

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...