Jirani aliyechonga dili kahama mtaa kwa hofu ya washabiki!
Udaku special, umevuja kutoka katika kambi ya FFU ughaibuni kuwa,
Mkuu wa Ngoma Africa band aka FFU,kamanda Ras Makunja atarudishiwa
mmoja ya ndege wawili aina ya Bundi aliyokuwa anawamiliki ,uamuzi
huo ulitolewa na idara ya uangalizi ya Oldenburg,huko ujerumani.
Mwishoni mwa mwezi wa nne mwaka huu,watu wasio julikana walifanikiwa
kuvunja banda walilokuwa wakiishi bundi wawili nyumbani (Anunnaki empire) kwa Ras Makunja na kuondoka na bundi hao wawili,baadaye
ndege hao walipatikana katika idara ya uangalizi wa wanyama,na mmoja
wao alirudishwa Amerika ya kusini.
lakini mwanzoni wa mwezi julai idara
ya wanyama imeamua kumurudisha ndege aina ya Bundi mwenye jina la Udi Udi kwa mmiliki wake ambaye ni mwanamuziki kamanda mkuu Ras Makunja.
Lakini inasemekana kuwa familia ya Kamanda imemtilingia ngumu baba mwenye nyumba kwa kumwambia Bundi hao wasiwekwe ndani ya nyumba bali nje ! .Pia jirani ya Ras Makunja aliyebebeshwa lawama za kuwa ndiye aliyechonga dila na kusababisha Bundi wakamanda wachukuliwe ,Jirani kahama mtaa kwa kuofia baadhi ya washabiki uwenda wakamletea tafrani, Tunamtafuta Kamanda Ras Makunja lakini
simu kazima
hiii! Kikamanda ketu ras makunja wamekurudishia bundi wako! sasa naona tour zitakuwa za nguvu sasa
ReplyDeletejirani lazima ahame mtaa kwa tabia za washabiki wa ffu
ReplyDeletekamanda sijakusikia siku nyingi sana,
ReplyDeleteulikuwa umejichimbia kambini au?
Kamanda nakujulisha kuwa waziri mkuu kishakupeni ruhusa ya kupereka virungu popote panapihitajika muziki
ReplyDeleteKamanda wale bundi heti uliachiwa na Ayesha G?
ReplyDeletemkuu kamanda ras makunja nikuulize kitu hivi,hii amri umliopewa na waziri mkuu,mtaichukuliaje ?
ReplyDeletebaba mkuu wa kikosi kazi,mfalume wa viumbe anunnaki,sasa watu wanafuga kasuku wewe unafuga bundi! au ndio unakataa wageni nyumbani
ReplyDeleteKamanda tafuta gwanda zako bwana, siyo mambo ya drug and drop.
ReplyDeleteKamanda waliokuchukulia bundi wako kwanini hukupiga? si mkipewa ruhusa kupiga? au mliogopa nguvu za umma?
ReplyDeleteHahahahaha!
ReplyDeleteAma kweli Kamanda Ras Makunja Mkonongo haachi asili yake popote aendapo, ni kuwa unawakilisha Afrika kikweli kweli huko,
Hadi BUNDI wa Tambiko unaye unafuga?
Kamanda Ras Makunja unatakiwa zaidi uende KIDIJITALI!
ReplyDeleteNi kuwa kuanzia sasa unatakiwa uwavalishe ELECTRONIC CHIP hao Bundi wako ili wakiibiwa ujue jinsi ya kuwa track na kuwapata!
Kamanda Makujnas,
ReplyDeleteSio bure!, huyo Jirani yako kama sio M-Benin, atakuwa M-Ghana, M-Guinea,Mu-Ivory Coast, M-Mali,M-Burkina Be wa Burkina Fasso ama M-Senegal wa West Afrika na inawezekana atakuwa na Imani za Kishirikina kwa kuweweseka baada ya kuona NDEGE BUNDI YUPO MJENGONI MWAKO ndani!
Mnacheza na West Africa?
Mwanawane Majuu kwa Kweli Demokrasia,Ubinaadamu na Haki ipo haswa.
ReplyDeleteYaani mtu unapoteza Bundi Serikali na Manispaa na Serikali za Mitaa wanahakikisha Haki inatendeka na unarudihsiwa ndege wako?
Bongo acha Bundi kupotea ndio hupati kabisa akipotea ukimpata atakuwa ni Marekemu zamaniiii, ile poteza Paka au Kuku oune kama utampata tena!
Ras Makunja utadhani kama yule Mfalme wa Mwisho wa Austria mwaka 1914.
ReplyDeleteHehehehe!
ReplyDeleteRas Makunjas ameona ya kuwa Mynama Bundi ametengwa sana na jamii kwa kuwa ni nadra sana ukute Bundi amefungwa !, labda iwe ni Kituo cha Utafiti wa Sayansi za Viumbe.
Hivyo baada ya Mwana wa Makunjas kuliona hilo ilibidi ampe hifadhi ya Kimaisha huyo Bundi akiwa kama Binaadamu anathamini utu wa Viumbe wote, kama alivyofanya Raisi wa Bolivia kupmatia Hifadhi Edward Snowden anatetafutwa na Marekani.