Mtendaji Mkuu wa Benki ya CRDB Dr. Charles Kimei akizungumza wakati wa uzinduzi wa upimaji wa Afya , zoezi litakalo endeshwa na Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa kazi (OSHA), kwenye matawi ya benki hiyo nchi nzima.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa kazi (OSHA) Dr. Akwilina Kayumba akielezea jinsi zoezi hilo litakalofanyika kwa wafanyakazi wa benki ya CRDB kwenye matawi yake yote nchi nzima, ikiwa ni mpango wa kuhakikisha wafanyakazi wanafanyakazi katika mazingira salama.
Mtendaji Mkuu wa Benki ya CRDB Dkt Charles Kimei akifanyiwa vipimo wakati wa zoezi la uzinduzi wa upimaji Afya kwa wafanyakazi wa benki ya CRDB, kwenye ofisi za makao makuu ya benki hiyo Jijini Dar es salaam
Madaktari toka OSHA wakichukua maelezo toka kwa wafanyakazi wa Benki ya CRDB, ikiwa ni mwanzo wa zoezi la upimaji Afya kwa wafanyakazi zaidi ya 2000 wa Benki ya CRDB ambao wanatarajiwa kupimwa Afya zao( Fitness to work) hivi karibuni kwenye matawi yote.
Hawa watu wa OSHA je wanatoa ushauri/tiba vipimo vikionyesha kuna kasoro au mapungufu kuhusu afya yako?
ReplyDeleteHili ni jambo zuri sana la kuhamasisha watumishi wa Taasisi kupima afya zao. naomba na Taasisi zingine zifanye zoezi kama hili.
ReplyDeleteConfidentiality is very important during provision of any excellent medical care, if Charles Kimei Bp is noted to be say 180/110, would you then inform him immediately and infront of others?
ReplyDelete