Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa ( wa nne kulia)akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wafanyabiashara wa mihogo katika soko la Ilala alipofanya ziara rasmi katika masoko ya Buguruni na Ilala kuangalia utofauti wa bei za bidhaa katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Mstahiki Meya aliwaasa wafanyabiashara kutokupandisha bei ya bidhaa mbalimbali wakati mwezi mtukufu wa Ramadhani ili kuwawezesha Waislamu wa mkoa wa Dar kuwa na mfungo mwema na wao pia kupata Thawabu kwa Mwenyezi Mungu kwani watawezesha hata wale wenye kipato cha chini kumudu bei ya bidhaa zinazotengeneza futari. Mh. Silaa amewatembelea wafanyabiashara katika masoko kuangalia uwiano wa bei katika masoko hayo.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akiendelea na ziara yake kwenye masoko katika halmashauri yake ya Ilala akiwa ameambatana maafisa wa mbalimbali wa Manispaa ya Ilala.
Hongera Mstahiki Meya Silaa kwa kuwajali wananchi wa Halmashauri yako.
ReplyDeleteKutembelea masoko/kuangalia bei za bidhaa mbalmbali ni jambo moja, lakini kuleta mabadiliko ya hizo bidhaa hadi zishuke ziwe bei nafuu ni jambo lingine. Sioni uwezekano wa wafanya biashara kushusha bei kwa sababu tu eti wametembelewa na Meya, mamlaka zinahitaji mikakati madhubuti ya muda mrefu ili kudhibiti bei kwa maslahi ya walaji, vinginevyo ziara kama hizi hazitakuwa na tija kwa wananchi, ni kama kiini macho na kuuza sura tu, wakati wafanya waroho wataendelea kupeta tu......
ReplyDeleteZiara ya kuangalia bei?huu ni utani,pls focus na kazi sio huu usanii,na angalia hapo unapopita kuchafu ile mbaya...ndio kazi yako hiyo kufanya mji msafi,elimu,ulinzi,maji etc lakini sio huo usanii!!
ReplyDeleteSijui nn? Maana ya uongozi yaani kiongozi mwenye jukumu la kusimamia usafi lakini yeye mwenyeeeewe ndio anapita juu ya takataka watoweni viongozi wajinga kama hao, hayo ndio mambo ya kuyaweka kwenye KATIBA MPYA.
ReplyDeleteHuo si uchafu ni majani ya migomba yanayofungashia bidhaa nakumbuka kwamba wakimaliza biashara jioni kuna mtu anasafisha mazingira hayo na hiyo ni asubuhi we mdau vipi??? uchafu hujui kwamba hapo ni sokoni na watu wako busy kushusha mizigo na bidhaa mpya ushamba tu na chuki binafsi Jerry Silaa anastahili pongezi ni kiongozi ambaye hataki watu wajinga na uzembe mimi nimekaa naye nishashuhudia anavyowawajibisha watendaji wake usione kaenda kuuza sura...... achana na kupandikiza chuki.
ReplyDeleteNyie mnaozungumza mambo ya usafi bongo bado mna moyo, jana nimesoma gazetini yule waziri aliyezifungia baadhi ya hoteli kwa kosa la kuchafua mazingira akisema amezinyooshea mikono halmashauri zote za jiji za kushindwa kuziweka ktk hali ya usafi halmashauri zao, huyu ni waziri mwenye dhamana.
ReplyDelete