Ankal Michuzi, za leo na pole na ugeni mzito wa Obama na Bush
Mie nna shida moja naomba wadau wa blog yetu ya jamii isiyo na mfanowe wanisaidie kama itawezekana. Maana naumbuka mwenzenu.
Ni hivi; mie ni kijana wa kiume wa miaka 30 na ushee hivi, naishi Tanga, Makorora. Nashukuru kibarua ninacho na hela ya kubadili mboga havinipi shida kiviiiile. Tatizo linakuja pale ninapokuwa naongea na wenzangu...Mvua ya denda hunitoka kila nnapotamka maneno, kiasi cha kuwakera wenzangu. Yaani yanibidi niwekage mkono mbele ya mdomon wakati naongea, ama sivyo naogesha wadau kwa denda.Isitoshe nna mpango wa kuoa karibuni, sasa hata sijui itakuwaje endapo shida hii itaendelea.
Je wadau wenzangu kuna dawa ya mvua ya denda? Ama nifanyeje ili nami niwe kama wengine? Kama mswaki napiga sana tu, tena mara mbili kwa siku - ninapoamka na wakati wa kulala. Kilaji napata mara moja moja siku za wikiendi, na kila mlo namaliziaga na matunda.
Naomba msaada nduguzanguni, niko chini ya miguu yenu maana NAUMBUKA!
Mdau wa Makorora


Pole sana, ila kwa sababu karibu unaoa basi usiwe na noma, ukishao utakuwa unampiga denda mkeo kila siku hivyo utaishiwa na denda na hutoweza kuwavurumishia dendaz innocent bystanders.
ReplyDeleteMdau Makorora naomba utuwekee video tuone hiyo khari inayokusibu.
ReplyDeleteTunaweza kuwaonyesha wataaramu na Wakatoa Ushairi ni Hatua gani Uchukue hee.
Tafuta Camera kisha anza Kurekodi halafu mrushie Brother Michuzi Ili aturushie.
Kama unaona Aibu kufanya hivyo
Usirekodi Uso wako , Bali Mdomo tu unatosha.
Ahsante
Pole sana mwana wa Makorora
ReplyDeleteKAMA UNAMAPENGO, KAZIBE. KAMA UNA MWANYA AU MIANYA BASI SAFARI NI NDEFU. CHA MSINGI NI KUWEKA UMBALI WA KUTOSHA KATI YAKO NA MSIKILIZAJI. TUANZIE HAPO KWANZA.
KILA LA KHERI NDUGU YANGU.
Nenda kamweleze daktrari matatizo yako kama ulivyotueleza sisi.
ReplyDeletepole sana mie nadhani nenda kamuone Dr. hapa watakuletea uzushi tu
ReplyDeletehehhehe.. Sipati picha tatizo lilivyo kwenye kiwango cha Lami..
ReplyDelete
ReplyDeletePOLE SAAANA NDUGU, JIFUNZE KUONGEA TARATIBU NA USIJAZE MATE MDOMONI.
MENO YAKO YAMEKAAJE? KAMA YANA NAFASI SANA BASI HII NDIO SABABISHO. JITAHIDI KUONGEA TARATIBU USIPAAZE SAUTI. KAMA MENO SAWA NA HUNA MAPENGO/MIANYA BASI LABDA MENO YAMEKAA VIBAYA. WENGINE WANAVAA BRACES KUYAREKEBISHA. ONGEA NA DENTIST MWENYE UTAALAMU.
ReplyDeleteMaelezo yako yanatatanisha, umefanya iwe vigumu kuelewa maana ya hilo neno DENDA ulilotumia kama ulikusudia ni (slang ya) busu au ni ute wa mate yaani kama vile udenda wa mtoto au ni vicheche (vichachicho) vya mate. Mimi dhana yangu ni unamaanisha vicheche vya mate na ushauri nilionao ni kukinga mkono kila unapoongea.
ReplyDeletewasiliana na huyu ndugu macha wa UK anaetoa mada zake kwenye hii blogu. huwa ana maujanja mengi sana ya kimaisha kama mazoezi ya kupumua, nk
ReplyDelete