Ndugu watanzania popote mlipo tunaomba uweke sahihi yako ili kutuzia tozo la kodi kwa watanzania katika line za simu.
Tafadhali bofa kwenye hiyo link na utapata maelekezo ya kufanya katika kuweka sahihi yako ili tupeleke malalamiko yetu katika bunge la Tanzania. Asanteni kwa ushirikiano wenu.



BOFYA LINK HIYO HAPA CHINI KISHA FUATA MAELEKEZO
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 16, 2013

    Wazo zuri je kwa wale wasiotumia mtandao, ambao ndio wengi watasaini wapi?

    ReplyDelete
  2. iskitogo@gmail.comJuly 16, 2013

    Sipingi utashi wa mtu binafsi, lakini sikubaliani na wazo la kupinga kodi hii. Ukiangalia fedha nyingi inayotokana na uwepo wa simu za mikononi zinavunwa kutoka kwa hao mnaosema ni wananchi wa vijijini baada ya kuuza pamba, kahawa, mahindi, majarage, nk na fedha hizo zinakwenda nje ya Tanzania kwa waliowekeza vitega uchumi hivyo. Ikiwa mtu mmoja anaweza kutumia zaidi ya 20,000/= kwenye simu moja kwanini basi tusitumie nguvu walau kidogo tu kwa kuelekeza matumizi mazuri na sahihi ya kodi hiyo kwa manufaa ya yetu wenyewe? Sioni mantiki ya kukata kulipa kodi ilhali sehemu kubwa ya fedha zinazopatika kwenye huduma ghali kabisa ya simu Tanzania zinakwenda nje ya nchi na hazimsaidii mwananchi? Afterall kodi hii si ya lazima, inawahusu wale ambao wanatumia huduma ya simu ya mkononi. Tupende kulipa kodi kwa ajili ya maendeleo yetu. Kila siku tunalalamika kwamba bajeti yetu ni tegemezi kumbe hata kulipa kodi kupunguza utegemezi wa bajeti hatutaki. I decline to sign this petition, kodi ni muhimu kwa maendeleo yetu, Tupiganie fedha za kodi zitumike ipasavyo. Kutokulipa hatumkomoi mtu bali tunajikomoa wenyewe.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 16, 2013

    Tanzania haijawahi kusikiliza kilio cha wananchi na kubadilisha bajeti yake, sasa tukisaini itasaidia nini? Tuliwahi kuambiwa ikibidi tule majani...... si itakuwa sawa na kumpigia mbuzi kengele!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 16, 2013

    Viongozi wa tz wafikirie walala hoi. Mpango yenu inabezi kwa wenye nacho katika kuweka mikakati.

    Nilisikia wamepanga kima cha chini cha mishahara kwa wtumishi wa ndani ni shs 50,000.00 . je mwenye kufanyiwa kazi anabangaiza kwa shs 200000 kwa mwezi. Viongozi wanataka kusema huyo house girl atumie robo nzima wakati kilakitu wanatumia wote pale nyumbani?

    Huu mpango unawafaa wenye mihela na ndio walioweka mkakati huu.

    Naomba hata wanaowateua viongozi wateue wenye busara. hawa mbumbumbu watatupeleka kubaya

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 16, 2013

    na kuıshi bila kodi uchumi hauwezi kukua...unataka ku spend lipa kodi.ungesema angalau wapunguze kidogo kodi hapo ungekua poa lakını sıo kutokulıpa kabisa..ni wakati kubadilika watanzania na kua na fikra mpya za kimaendeleo.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 16, 2013

    kweli kweli mawazo ya watanzania wengine kama huyo iskitongo na wewewe anony unayesema bila kulipa kodi nchi haiwezi kupata maendeleo ni ya ajabu na ya kushangaza. jaribu kufanya tathmini ni watanzania wangapi wenye simu ambao wanatumia zaidi ya shiling 2000 kwa mwezi kwenye simu zao. jaribu kutafiti ni kwa nini wauza vocha wameweka hadi za shilingi 500 ambazo ndo zinauzika. acheni ubinafsi. ukijiona una hela sana na ambayo in actual fact ni ya wizi kwani najua mshahara wako haukupi excess kiasi hicho, usione ni sawa kuumiza wengine.

    kama wanataka kodi kwa nini wasiache kusamehe kodi ambayo ni hela nyingi sana? kwa nini wasiwatoze kodi makampuni ya utalii ambayo hayalipi kodi. mimi kwa ushauri wangu kama kodi ya sim card inatozwa basi iwe kwa watu wenye matumizi ya zaidi ya shilingi 10,000.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 16, 2013

    Nahayo matamasha ya makampuni ya simu ya kujitangaza je! Makampuni ya simu yafidie hiyo kodi na sio kuwaumiza wauza pamba, kahawa mahindi nk maana hawa wanakijiji unakuta kwa mwezi bajeti yake ya simu ni Tsh 1000 au chini yeye ni kuweka hela ili abipu na kupokea simu.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 17, 2013

    Hizi kodi tunalipa kila mara. Mie binafsi nimeajuriwa niaka 40 iliyopita kila mwezi nalipa kodi kwa maendeleo ya taifa . Lakini mpaka leo shida ya maji ndo kwanza, umeme usiseme, ujamabazi mama mama n.k

    Bora tuzikatae hazitusaidii zinasaidia vigogo na familia zao

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...