Habari Uncle michuzi,
Kwa manufaa ya wazazi na watanzania woote waliofikiwa na habari ya kwamba mwanafunzi mtanzania mjini Bandar Sunway, Malaysia, amekamatwa na 8kg za heroin kama ilivyo kwenye source of news katika link hii hapa chini:
Sisi kama wanafunzi Watanzania tunao ishi Bandar Sunway kwanza tulishangazwa na taarifa hizi na kila tukiulizana ni nani huyo aliekamatwa tunakosa jibu kwani kwa idadi ndogo na wengi kufahamiana kama marafiki Watanzania tunaona woote tuko sawa na hakuna anaekosekana
Jana nilikua na case yangu katika kituo cha police Sunway ambapo mtu huyo anaesema ni mtanzania alifikishwa na police walipoona nina passport ya Tanzania waliniuliza " you Tanzania soo bad now days" nilipo muuliza sababu walianza kumwaga sera jinsi tunavyo smuggle drugs pia alinionyesha picha zilizokua kwenye notice board za watu waliokamatwa Ridzuan Condominium siku hiyo walipo fanya raid akiwamo huyo anaesema ni mtanzania
Ukweli ni kwamba nilishangazwa sana kwani mtuhumiwa kwa sura nimewahi kumuona Ridzuan lakini sio MTANZANIA kabisaaa na hakuna anaemfahamu
Kibaya zaidi na cha kushangaza ni kwamba amekutwa na passport ya TZ alafu na ATM card ya Zenith Bank kuona hilo navyojua hakuna zenith bank Tanzania ipo Nigeria peke yake mpaka hapo jibu nikalipata.
Kinacho uma zaidi ni kwamba wazazi wetu walipo pata hizo taarifa walianza kusema tukae mbali kati yetu sisi watanzania kwani imani imesha pungua kumbe ni mjinga mmoja kaleta haya yoote kwa kweli ina uma sanaaaa na inakeraa!
Mie ninge suggest kama inawezekana immigration wabadilishe passport za Tanzania na kupata aina mpya ambayo hawa wajinga hawataweza kuwa nazo na hata kama watafanya fake made itakua ni ngumu sana kuziweka kwenye circulation ili kuepuka jinsi tunavyo chafuliwa na kupakwa matope duniani kote.
Student Segi College Sunway
Wanachafua jina la TZ sana! wapo wengi hadi Waburundi wanauza unga lakini wanatumia passport za Ki TZ kusini mwa Afrika!
ReplyDeleteTatizo liliopo mdogo wangu ni kwamba hata tukibadilisha pass za Tanzania idara ya Uhamiaji isipokaa sawa itakuwa ni kazi bure! Bahati mbaya ni kwamba hawa unaowaita wajinga wanakuja hapa wanaruhusiwa kukaa (Na uhamiaji) wanafanya mipango wanapokuwa hapa na kupata pass za Tanzania ( kutoka Uhamiaji)
ReplyDeleteKwa hiyo tatizo nadhani ni kubwa zaidi katika Idara yetu ya uhamiaji na hilo ni rahisi tu kuthibitisha kama uhamiaji watakuwa serious kutaka kutatua tatizo, hata hiyo pasi aliyokamatwa nayo huyo mtu ni rahisi kujua kama imetolewa hapa kwetu au la! ikithibitika kwamba imeghushiwa kwingine basi tumepona na hayo mapendekezo yako yanaweza kuwa valid otherwise kama itaonekena ni pasi halali iliyotilewa isivyo halali basi tatizo litakuwa ni kwa idara ya Uhamiaji jambo ambalo mimi nataka kuamini kwamba inawezekana wanazipata hapa hapa pamoja na kwamba sina hakika na hilo lakini kwa kuwa ni jambo linalosemwa basi ili kunusuru Taifa na wananchi wa nchi hii tunatakiwa kulifanyia kazi kwa makini kwani malalamiko ya pasi zetu kutolewa kama njugu kwa raia na wasio raia hajaanza leo
Matokeo ya rushwa kuitawala nchi. Wapo maafisa uhamiaji wengi na wengine wenye vyeo vya juu sana ambao kwa ubinafsi wao huwatengenezea pass wageni baada ya kupewa rushwa. Passport za kitanzania huuzwa kati ya mil 3 hadi saba za kitanzania. So tusiwalaumu wageni, wachawi ni sisi wenyewe na viongozi wetu. Nimewahi shuhudia mchina Zanzibar akiwa na pass ya Tanzania we unashangaa mpopo?
DeleteJamani tulishasema huko nyuma,kuwa tanzania kuna matatizo ya utawala,hakuna kuwajibika,naomba mungu ifike siku hata viongozi wetu wazuiwe kusafiri au wasumbuliwe kwa kusachiwa kama sisi tunavyopata tabu.
ReplyDeletePassport zetu zipo nje nje tu kila mtu anayo kadri anavyotaka tena watu wa nje ndio wanapata kwa urahisi sana.kisa wana pesa.uhamiaji wachunguzwe na kuwajibishwa
Kama anamiliki paspoti halisi ya Tanzania basi ni Mtanzania! simple.
ReplyDelete..poleni.
Ndugu yangu mwanafunzi wa Malaysia,
ReplyDeleteKama umoja wa wanafunzi wa Tanzania huko,itakuwa vema kama mtaweza kufuwasiliana na police kujiridhisha kama kweli huyo ni Mtanzania,ili nao wajue kuwa huyo mtu si raia wa Tanzania.
Wanaochafua jina la Tanzania ni wengine,lakini wanaoumia ni Watanzania,manake wao wanaangalia tu Passport. Nafikiri kuna haja ya kuwa na sreening kubwa sana kuajiri watu kwenye idara nyeti kama Uhamiaji!
Inaudhi sana!
watu wanashangaza wanavyosema wankamatwa na sembe sio watanzania .kuwa na benki card ya nchi nyingine sio tija ya kumfanya mtu kuwa sio mtanzania .kwani si anapasport ya Tanzania .pengine aliwahi kuishi huko Nigeria before.wafungwa walioandika barua kutoka Hongkong si watanzania .Mackubi aliyekamatwa Marekani naye ni Mtanzania pure tena an tour campany hapa bongo na amesoma huko America .huyu rasta Edwin anyeishi Greece waliayemkamta juzi naye ni mtanzania piwa ,Agnes na melisa nao ni watanzania piwa.Tusianze kusingizia watu wanatumia pass zetu ili kufisha ukweli kwamba tatizo ni vijana wa kitanzania kuwa na tamaa ya maisha ya utajiri wa haraka hivyo wanajiingiza kwenye madawa. soo waache wanyongwe tu au wapewe hicho kifungo cha maisha iwe fundisho.lakini siyo kusema eti siyo watanzania.haya mabondia wakitanznia waliyofungwa maurtania, Binti Kiziwi siyo mtanzania?wacha tuu wakamatwe .watakoma tena wangetaja na hawa wanaowatuma tuu au wanakonunua .
ReplyDeletewenu mpiga box hodari kutoka Uk
Ndugu wana blog,ninachoona mimi hapa pana matatizo mawilia ama zaidi. Tatizo mama ni rushwa ambayo hata Biblia inasema hupofua macho.Kuna tatizo la rushwa ambalo linapelekea kutoa passport kama vile ni jambo dogo sana na pia kupelekea mtandao wa unga 'usiguswe'.Ni kweli kwamba Tanzani sasa ipo kwenye ramani ya dunia katika madawa ya kulevya hii ikiwa inafanywa na watanzania wa ukweli na wale waliouziwa utanzania.Lakini lazima tukubali kwamba passport za Tanzania zimeichafua nchi yetu sana,na ingawa sina takwimu naweza kusema kwamba hawa waliokamatwa na madawa,nusu ni watanzania wa kununua. Niliwahi kuandika tena kuhusu passport za Tanzania na Malawi zinavyomilikiwa na watu wengi hasa wa nchi za Africa Magharibi.Zamani airport mtanzania alikuwa hakaguliwa kwa umakini mkubwa lakini sasa hatuaminiki. Uhamiaji kuna tatizo kuhusu passport na hili lazima lishughulikiwa kwa haraka.
ReplyDeleteTanzania is no longer safe, kwa kweli madawa ya kulevya ni watanzania wenyewe wanafanya hiyo biashara! Tusisingizie wana-nigeria jamani. Kama wapo wachache sana wanaotumia pport za Tz. ila kwa waliokamatwa wengi ni WaTz. Ni aibu sana kwa Taifa la Tanzania. Mungu aiepushe na mabalaa ya madawa na kulevya na pia tindikali na kutapaa kwa silaha nje nje na kuuana.
ReplyDeleteKila kitu kiboyu Tanzania. Raisi mwenyewe kakili kuwa hata wageni kutoka Rwanda wakihonga ng`ombe wawili tu kwa serikali (za vijiji) wanaruhusiwa kuingia kuishi na kufanya mambo wanayotaka Tanzania.
ReplyDeleteTatizo la kuuza passport za Tanzania halijaanza leo. Hili tatizo mimi nalijua tangu nasoma sekondari (Miaka 20 iliyopita). Kuna wahindi na watu wa mataifa mengine huko Canada na nchi zingine ambao waliingia kwenye nchi hizo kama watanzania wakati hata kiswahili hawajui.
Ukweli ni kwamba Tanzania inaendeshwa kama boya. Ni sandakalawe isiyo na manunuzi!
UNAPIMA URAIA KWA KUJUANA, SURA NA CREDIT CARD? ANYWAY, MASOGANGE SIDHANI KAMA NI WA NIGERIA!
ReplyDeleteTunatia aibu jamani si kitoto. Niko Finland nimeshuhudia kwa macho siku nimepata kazi kampuni inaitwa L&T, nimekuta kuna mtu ameandikwa jina ofisini kuwa ni Mtanzania. Tukipokutana siku moja accent yake ya ki west na hasemi Kiswahili!! Baada ya siku hiyo sikumwona tena hadi leo niko hapo mwaka wa pili sasa!!!
ReplyDeleteTAIFA LINAANGAMIA KWA SABAU YA RUSHWA NA KUKOSA SHERIA ZAINAZOBANA NA KUTOKUWA NA MAADILI KWA VIONGOZI.WIZI WA MALI ZA UMMA UMEKITHIRI NA VIJANA NAO WAKIONA HIVYO NA HUKU HAWANA NAFASI YA KUPATA WANABUNI NJIA ZINGINE KAMA HIVYO ILI NA WAO WATAJIRIKE HARAKA IWEZEKANAVYO.
ReplyDeleteRUSWA NI HATARIRUSHWA NI HATARI NA NDO CHANZO CHA YOTE HAYA.
JAMANI JAMANI HUYO BWANA MWANAFUNZI NAONA KAMA NI MGENI KATIKA MAMBO YA KUSAFIRI. MIMI NI MTANZANIA MAMBAYE NAISHI HAPA NORWAY , KWA KWELI KUSADIKI KWA THOMAS NI KUJIONEA,,! KUNA MTU NAMFAHAMU HAPA TROMSO KWA MIAKA KAM MIWILI HIVI NA KILA WAKATI NASALIMIANA NAYE NIKAMMULIZA NI MTU WA WAPI YEYE AKANMBIA NI M NAGERIA SIKU MOJA NIKAMKUITA MIGRATION ANAONGEZEWA UDA WA KUISHI HAPA KUONA PASI YAKE NI YA TANZANIA! KWA KWELI NILISHUTUKA SANA NILIPOMUULIZA KAMA ALIWAHI NAMBIA YEYE NI MNAGERIA AKASEMA ILIKUWA GERESHA PASI YAKE NI FEKI ILIIPATA TANZANIA KWA MIPANGO BASI NIKAMUACHA AENDELEE NA MAISHA YAKE KWANI MIMI SIO MTU WA KUMZIBIA RIZIKI YAKE. SASA WARUNDI, WANYARWANDA, WA GHANA, WASOMALI NDIO USISEME
ReplyDeleteSASA KILA ANAEKOROFISHA HAPA ANAONEKANA NI MTANZANIA LAKINI NO SWEAT TUSHA ZOEA
waamsheni hapo ubalozini,wamelala sana, waambieni wakanushe kwenye vyombo vya habari mapema kwa gharama zozote,nilipokuwa huko niliwachukia sana wanigeria na dada zetu ndo wanawababaikia, kumbe akikodishiwa gari kwa wiki hajui anabebeshwa unga akiitwa club watu wanauza mzigo,jaribuni kuwaelewesha hao dada zetu,wema alishabeba sana ila sijui kama alijua ilo
ReplyDelete