Mkurugenzi wa Masoko Utafiti Huduma kwa Wateja wa benki ya CRDB, Tully Mwambapa akipeana mkono na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati wa hafla hiyo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akiingiza kadi kwenye mashine ya kutolea fedha wakati wa uzinduzi wa kadi mpya ya Tembo Card China Union Pay ambayo itamuwezesha mteja wa benki ya crdb kufanya malipo yake akiwa China. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, CRDB, Martin Mmari na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk. Charles Kimei (katikati)
Waziri Mkuu Mizengo Pinda, (kushoto), Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Dk. Mary Nagu, balozi wa China, Dk. Lu Youqing, Rais wa China UnionPay, Xu Luoude wakizindua kadi mpya ya Tembo Card China UnionPay, itakayomuwezesha mteja wa benki ya crdb kufanya malipo yake akiwa China. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...