Swahili TV inakuletea kipindi maalumu sherehe za watanzania waishio DC, Maryland na Virginia walipokutana kwa siku maalum ya familia (Picnic Day) iliyofanyika Wheaton Reginal Park, MD, jumamosi August 17, 2013. Muhimu zaidi waliweza pia kuchangia rasimu ya marekebisho ya katiba mpya ya Tanzania. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mambo yooote yaliyoongelewe katika video hii fupi nimepata picha kuwa nyie huko US swala linalowatatiza katika katiba mpya, ni swala la Dual citizenship. Yaani mnataka mshike yote kwa wakati mmoja!..mshika mbili moja humpotoka, na kwa jinsi ninavyofahamu up to 95 per cent mlioko hapo USA legally Zaidi ya 5yrs tayari mna uraia wa US, na pia kuwa passport zenu za Kibongo mnazo. Kuna Watanzania kama million 2-5 ambao wanaishi nje ya TZ na hao wanalipa kodi kwenye inchi hizo wanazoishi, hivyo ya nini kuwa na idadi kubwa ya Watanzania wakati physically hawapo.Na ukiangalia demographic data za Tanzania last moth utaona kuwa tuko 48,261,942 (July 2013 estimate) na kwa population groth ya 2.85% (2012 est. ) Birth rate, 37.7 ... Death rate, 8.6 deaths/1,000 population (July 2012 est.) kufikia mwaka 2016 population itakuwa 51 million. Hivyo kwa maoni yanggu kwa inchi zinazoendelea TZ ikiwemo ni mapema sana kuruhusu uraia pacha.Hatutaki kuwa na idadi ya Watanzania isiyo sahihi kwani itatupa mahesabu yasiyo sahihi katika kupanga programs za maendeleo, mfano tujenge shule ngapi,vyuo vikuu Hospitals ngapi,wataalamu wangapi wahahitajika..waalimu,madaktari n.k
    Je swala la Muungano ktk katiba mpya mlisemaje? Elimu, dini,haki za jinsia (mwanamke na mwanaume) etc

    ReplyDelete
  2. Mdau wa kwanza,hoja zako hazina mshiko,tuwe open mind. Moja,kujua idadi ya watu waliopo nchini na wenye dual citizenship,ni record mbili tofauti,hilo linawezekana kwenye digital era,so wazo lako la budget,sensa halina mshiko. Pili,tuna wataalam fani nyingi,nina hakika tukiwa na uazi ktk maeneo ya ujuzi,uwekezaji,tutapata ujuzi,kuongeza ajira maana mkaazi wa ulaya/marekani wataajiri wawakilishi wao na kuwapa ujuzi. Tatu, security ya nchi yangu na ya ugenini inakua sababu ya ukaribu wa wananchi wao. Nne,watoto wa watanzania waliozaliwa in 21st century,wako wengi,ni raia wa ugenini,wanachokula,wanaongea,na kuishi kwa maadili ya nyumbani,leo unamwambia hutambuliwi kama mwafrika,jina lake,nywele zake,karatasi za kujaza asilia inamwita mwafrika,mzazi unaeleza vipi? Tunawaomba wajumbe wa katiba wawe ma "empathy" kwa dakika 1, stop and think,can be ur child,grandkids. Hawa ndio watakaokuwa future leaders wa ughaibuni. Je,ukiwakataa leo,akijakuwa kiongozi ndio mtaanza kuwaita ooh wa kwetu kama wakenya!!!?? Aibu!! Tafadhali hili jambo liangaliwe kwa kina. Nakubali,watu wame abuse kwa kuwa na uraia miwili,lakini wengi wao sio origins. Nawaongelea hapa ni watz wazawa,wakaenda ughaibuni,wakawa wakaazi,na wamejaaliwa kuwa na watoto huko mbali. Tuwaulize jirani zetu waliopitisha hii sheria na mpaka leo inawanufaishaje,nchi nyingi; Kenya,Uganda,Burundi,Mozambique,Nigeria,Ghana,Angola,South Africa,Namibia,Lesotho,Sierra Leone,Djibouti,Eritrea,Ivory Coast,etc.....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...