Pichani juu askari wakikagua mwili wa Erasto Msuya, mmoja wa Wafanyabiasha wakubwa wa Madini jijini Arusha aliyejulikana ambaye pia ni mmiliki wa SG HOTEL mkoani humo, baada ya kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi na kufa papo hapo.
Kwa mujibu wa baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa mfanya biashara huyo alifariki dunia mara baada ya majibishano ya risasi baina ya majambazi hayo na mfanya biashara huyo ambapo alizidiwa nguvu na kupigwa risasi na kufariki dunia
Habari zinaeleza na kubainisha zaidi kuwa Marehemu alikuwa akitokea KIA kwenda BOMA ambako alikuwa ameitwa na watu (ambao hawakujulikana mara moja) ili wakafanye biashara.
Habari zaidi tuvute subra kidoogo,
tutazidi kufahamishana kadiri ya taarifa zitakapokuwa zikiingia.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi-Amen.
Kuna haja ya jeshi la polisi kuongeza nguvu katika mkoa wa Arusha kutokana na matukio ya uhalifu yanayotokea mkoani humo mara kwa mara
ReplyDeleteI did loose my uncle Edward Shaba (Mtoto wa marehemu speaker wa bunge Austin shaba ) alipigwa risasi mambo haya ya madini
ReplyDeleteano wa 2.
ReplyDeletesorry you did loose your anko to me Edward Shaba was one of my best friends.GOD rest him in peace.
mikidadi-denmark
Hali si shwari kabisa hapa nchini. Huu wimbo wa ' Amani na Utulivu' has been overtaken by events. Nchi hii sasa ni ya kibedui. Jeshi la Polisi ni usanii mtupu, halafu wanadai wana taarifa za ' kiintelijensia' , when it comes to opposition.
ReplyDeleteHakuna majibu kabisa katika matukio mengi ya ki halifu. Weledi uko wapi?
It's no longer kisiwa cha amani, wimbo huu uhitimishwe sasa.
Kule Zanzibar husema wanafanya utafiti wa Kisayansi na Tekelakujia.
ReplyDeletePolisi Migwanda kazi yao siasa tu na kulinda Chama.
Silaha zimezagaa mitaani.
Muhadhiri kapigwa chuo Kikuu kapigwa risasi. It is just tit for tat.
Yangelijiri Zanzibar matukio haya. Wangelituita Alqaida Zanzibar nzima.
Get serious now. Polisi wacheni siasa. Si kazi yenu.
Ni kawaida yetu wananchi kulaumu serikali lakini jee sisi kwa nafasi zetu tunashiriki vipi kulinda amani? Watu wanajua majambazi wanabaki kunyamaza na kuficha siri za wanaomiliki silaha kinyume na sheria. TUSHIRIKIANE JAAMANI HII KAZI YA KUFICHUA MAJAMBAZI SI YA POLISI PEKEYAKE
ReplyDeleteArusha has become chaotic jmn....pamekuwa km uwanja wa vita...leo mabomu kesho risasi....achilia mbali watu wa matabaka ya chini ambao wanauwa vinazimwa kimya kimya....enuf iz enuf....its about time that jeshi la polisi wnanchi na serikali kwa ujumla to something to change tht....bila ivo tunapokwenda c pazur
ReplyDeleteMay Mr. Msuya rest in eternal peace!!
Pole sana kwa wafiwa.
ReplyDeleteHawa watu watafutwe na wawe fundisho kwa wote wanaochukua uhai wa wenzao. Watu wanahenyeka, wao wanawaza jinsi ya kukunyang'anya, wao kujishughulisha hapana. Wanapenda mteremko.
Kwa Kuwa siku hizi namba za simu zimesajiliwa ni vizuri kutrace namba ya marehemu kwa service providers, wanaweza wakapata namba ya simu ya hayo majangili Kwani walimpigia wakutane sehemu hiyo wakati huo.
Hakuna haja ya kujisifia kuwa sisi ni watu wa amani kama mwendo ndo huu wa risasi, tindikali, mapanga, sumu, na unyanyasaji usioelezeka unaendelea kuwepo.
Naogopa jamani erasto umeondoka mapema sana
ReplyDeleteMungu akulaze mahali pema peponi
Wengi hawapeleki taarifa Polisi kwani at the end of day zoezi litakubadilikia nawe ukabambikwa uhalifu kwa lengo la kupata rushwa. Nasema hivi, Polisi kumeoza. Garbage in garbage out! Sub standards tupu na udhalimu katika jeshi hili. Wajipange kwani wananchi hawana Imani kabisa na jeshi hili. Ukweli ndio huo.
ReplyDelete