Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua Maonyesho ya Kongamano la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuadhimisha Siku ya Mabunge Duniani, kuhusu suala la Makazi. Kongamano hilo limefunguliwa leo Agosti 19, 2013 jijini Arusha. Kulia ni Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makzi, Prof. Anna Tibaijuka. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Kongamano la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuadhimisha Siku ya Mabunge Duniani, kuhusu suala la Makazi. Kongamano hilo limefunguliwa leo Agosti 19, 2013 jijini Arusha.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la Ukumbi wa Bunge la Afrika Mashariki, baada ya kufungua rasmi Kongamano la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuadhimisha Siku ya Mabunge Duniani, kuhusu suala la Makazi, lililofunguliwa leo Agosti 19, 2013 jijini Arusha
 
 Baadhi ya wabunge na wageni waliohudhuria ufunguzi wa Kongamano hilo leo, jijini Arusha.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja Masoko wa Kampuni ya Tree Ltd ya Arusha, Magdalena Ayo, kuhusu utengenezaji wa Majiko Bomba, wakati Makamu alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonyesho ya Kongamano la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuadhimisha Siku ya Mabunge Duniani, kuhusu suala la Makazi, lililofunguliwa leo Agosti 19, 2013 jijini Arusha. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki, wakati akiondoka baada ya kufungua rasmi Kongamano la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuadhimisha Siku ya Mabunge Duniani, kuhusu suala la Makazi, leo Agosti 19, 2013 jijini Arusha. 
Picha  ya pamoja

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...