20130818_161729_resized
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Chimbo School of Thought ambaye pia ni mtangazaji wa redio Clouds na TV Harris Kapiga wakati alipofika kwenye chimbo hilo kuzungumza na vijana baada ya kuitikia mwaliko kutoka kwa Mwenyekiti huyo.
20130818_162938_resized
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mwenyekiti wa Chimbo School of Thought ambaye pia ni mtangazaji wa redio Clouds na TV Harris Kapiga.
20130818_164446_resized
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akitema cheche kwa vijana na kuwatia moyo.
20130818_175056_resized
Mmoja wa vijana akimuuliza maswali Mstahiki Meya Jerry Silaa.

Na.Mwandishi wetu.

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akiwa katika ya nchi ya Ahadi Sinza Kamanyola amefunguka kuhusiana na namna gani kijana anaweza kuishi ndoto zake.

Moja ya mambo aliyoyazungumzia ni pamoja na kijana kujitambua na kujua nini hasa anataka na anapata vipi kwa maandalizi ya kutimiza nia yake.

Mh. Jerry pia amechambua mada hiyo kwa marefu na vijana kuonekana kumuelewa ipasavyo na hivyo kubaki kazi kwao kutekeleza na kuyafanyia kazi yale aliyoyazungumza, ikiwemo kujua lengo lao hasa ni nini na kujipima wanautayari wa kiasi gani katika kutekeleza hilo lengo na kubwa zaidi ni uthubutu wa kufanya jambo lenyewe.

Katika mazungumzo yake kilichowavutia vijana wengi zaidi ni pale alipowaeleza kuwa yeye Mstahiki alithubutu kugombea udiwani ndani ya kata ya Ukonga akiwa na umri wa miaka 23 na kufanikiwa kushinda.

Ni jambo la kujivujia kuwa na vijana hasa kama mstahiki Jerry Silaa ambaye pamoja na kuwa Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu ya Chama tawala cha CCM Taifa.

Pamoja na hayo Mh. Jerry Silaa amewaeleza vijana kutambua hizo ndoto ni za nani hasa na ni nani wakuzifanikisha kama si wenyewe.

Aidha, zaidi ya hapo amewaasa vijana kuwa na majibu ama matokeo ya kila wanalofanyia kazi "being result oriented" na kupata kile wanachokitaka kwa kuzingatia lengo pamoja na muda kiutendaji.
20130818_183833_resized
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa katika picha ya pamoja na vijana waliojitokeza kumsikiliza wakati akifunguka kuhusuiana na namna gani kijana anaweza kuishi ndoto yake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Blog ya Jamii:Naomba niende nje ya Mada Kidogo.HALMASHAURI YA WILAYA YA TEMEKE-Kuna hii barabara ya Kilwa.Kutoka pale round about sijui ndiyo bandari/kurasini kuelekea Mivinjeni,Ufundi,nk.Kuna kipindi fulani MKUU wa nchi alipanda miti pale.Miti ikamwagiliziwa wiki ya 1,2,3....kilichotokea baadae.....Ninavyotoka mara 1-1 kwenda huko "DUNIANI" sehemu kama zile 'WENZETU'wanajenga Seng'eng'e ili raia wasitakize na kuharibu vegetation(Ni kuvuka kwenye Zebra tu),na kuna watu wanalipwa kwa kumwagilia maji maua,miti nk..Yaani barabara zao zinapendeza kweli kweli.You cannot teach an old dog new tricks lakini..........

    David V

    ReplyDelete
  2. mjomba hicho kiti ulichokalia muheshimiwa uliyetembelewa na meya sio kiti cha shughuli za kiofisi ! hicho ni kiti cha meza ya kulia chakula majumbani..kitakupa matatizo ya mgongo sanaaa...tuache longo longo bongo....ofisini ni nzuri ila hicho kiti kinatoa dosari sana..vipi haukukujua ni kiti gani kinatumika ktk shughuli za kiofisi ? anayway, ujumbe wa huyo meya naukubali kabisa !! na hizo nondo dirishani mh !! sijuwi pakishika moto hapo utatoka vipi humo ndani !! I am just saying....

    ReplyDelete
  3. Wewe unayesema habari za nondo, unaishi wapi?na hata kama upo ughaibuni na umegoma kujenga kwenu, yakupasa ujue ujengaji wa ughaibuni na Bongoland ni vitu vi2 tofauti.
    Bila Nondo,unawaalika "Wajasiriamali" wa usiku na kufanya kazi yao iwe nyepesi.
    Ni kweli uwekaji wa nondo hivyo ni hatari pakitokea dharura ila "Ndipo kama nchi tulikofikia"

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...