KAMPUNI ya Msama Promotions imejipanga kutoa madawati kwa shule mbalimbali za msingi zilizoko Wilayani Kinondoni Jijini Dar es Salaam kabla ya mwaka 2014.
Akizungumza mwishoni mwa wiki , Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Alex Msama alisema ugawaji wa madawati hayo utakwenda sambamba na ugawaji wa sare na vifaa mbalimbali vya shule. Msama alisema hivi sasa ameunda kamati maalumu ya kutembelea shule ambazo zina upungufu wa madawati na vifaa vingine. Msama Promotions ni kampuni ambayo imesaidia jamii kwa muda mrefu, ambapo sasa imeamua kujikita katika suala la elimu.
Alisema mpaka sasa wameshatengeneza madawati yapatayo 50,000 na kwamba dhamira ya kampuni hiyo ni kuinua kiwango cha elimu katika Jiji la Dar es Salaam, ambapo kwa kuanzia wanaanzia katika wilaya ya Kinondoni.
“Kampuni ya Msama promotions imedhamiria kuwasaidia waanafunzi wa shule za msingi wasome kwenye mazingira mazuri ambayo yatafanikisha maendeleo yao na nchi kwa ujumla” alisema Msama.
Aliongeza kuwa ili kufanikisha mipango ya kusaidia elimu, hivi sasa kampuni hiyo iko kwenye mchakato wa kupata hati kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kimataifa cha kulelea watoto yatima na wasiojiweza. Kituo hicho kinatarajiwa kujengwa katika eneo walilopewa na Rais Jakaya Kikwete lililopo Pugu, jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...