Mtoto wa kike mwenye umri unaokadiriwa kuwa miaka 3 ama 4 anayesema anaitwa Manka ameokotwa leo na wasamaria wema maeneo ya Upanga jijini Dar es salaam na kupelekwaa katika kituo kidogo cha polisi cha Salender ambako hadi tunaenda mitamboni alikuwa amehifadhiwa hapo. Juhudi za kuwatafuta wazazi wake ama wanafamilia zinaendelea na wito umetolewa kwa yeyote anayemfahamu mtoto huyu ama wazazi wake aende kituoni hapo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Mungu asaidie jamani,katoto kazuri sana,sipati picha mamake Huko alipo.

    ReplyDelete
  2. ankal Michuzi,
    kama ndugu na wazazi wa mtoto hawakujitokeza basi unitafute mie mdogo wako,mtoto ajipatie mwanzo wa kwenda xull ya chekechekea au darasa la mwanzo,si mila zetu kuwaacha watoto wa ki-tanzania mitaani bila ya wazazi kuwatafuta.
    Mikidadi-Denmark

    ReplyDelete
  3. Kwanini mtoto mwenye umri mdogo kama huo apelekwe kituo cha polisi, wizara ya ustawi wa jamii na watoto iko wapi? au kama tulivyo zoea raisi [Jk] anatakiwa amchukue/aingilie?ningeomba wizara ya watoto ifutwe na wafanyakazi wafutwe kazi kwani kazi yao inafanywa na polisi,ambao wanatakiwa kulinda usalama wa watu nakukamata wahalifu siyo kulea watoto lini tutaendelea mr Kikwete?

    ReplyDelete
  4. Wewe unayetaka mtoto wa kumpeleka xull ya chekechea; nenda pale faya Dar-es-salaam utakuta watoto wamelala kando kando ya barabara hawana wenyewe. Chukua mmoja mpeleke xull.

    ReplyDelete
  5. KAKA KAMA HUYU MTOTO NDUGU HAWATAPATIKANA NAKUOMBA TUWASILIANE NIMPLEKE UK AKAJILIPUE APATE MAISHA MAPYA.MDAU LONDON

    ReplyDelete
  6. polisi ni mahali pa usalama(usalama wa raia)kumbuka pako wazi masaa 24,tofauti na ustawi wa jamii,baada ya hapo polisi ndio wanapaswa wamjulishe afisa ustawi wa jamii,(sidhani kwamba huwa wanafanya hivyo)lakini pa kuanzia ni polisi.Si kwamba amefanya kosa,la hasha ni kwa usalama tu,msiwaogope sana polisi jamani pamoja na kupewa ruksa ya kupiga na mtoto wa mkulima.

    ReplyDelete
  7. Che GuevaraAugust 20, 2013

    tatizo la wizara iliyo na jukumu kwa watoto hawa haina kiongozi mwenye utashi hata kidogo! Anaendeleza USWAHILI TU pale!

    Cha ajabu anabebwa tu !

    ReplyDelete
  8. Kwa nini na hao wa fire wasichukuliwe wapelekwe ustawi wa jamii????

    ReplyDelete
  9. Asante sana Ankal kwa kutoa habari na picha humu imesaidia wazazi wa huyu mtoto kupatikana,na nyote mlomuombea asanteni sana kwani alichukuliwa jana usiku na Manka Yuko salama sasa na wazazi wake.
    Carol Magessa

    ReplyDelete
  10. wa fire wapo pale at their parent's accord.

    ReplyDelete
  11. Such a beautiful Angel.... ALLAH amjaalie aungane na wazazi wake ...Anka tujulishe akishapatwa na wazazi wake tafadhal

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...