Teknoljia ya mstari wa goli ajili ya Ligi Kuu ya Uingereza imezinduliwa
leo na kusifiwa kama moja ya maendeleo muhimu toka sharia za soka ziwekwe na
kuanza kutumika miaka 150 iliyopita.
Teknolojia hiyo ijulikanayo kama ‘The
Hawk-eye’ (jicho la mwewe) inatumia kamera 14 ambazo zitatuma ujumbe ndani ya
sekunde moja katika saa ya mwamuzi pamoja na kifaa cha sikioni cha mawasiliano
mara tu mpira utapovuka mstari wa goli.
Watumiaji wa kwanza wa kifaa
hicho watakuwa timu za Manchester United na Wigan Jumapili ijayo katika mchezo
wao wa ngao ya hisani kuashiria kuanza rasmi kwa ligi hiyo katika uwanja wa
Wembley.
Cheki Video hii ya jinsi kifaa hicho kitavyofanya kazi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...