Sheikh Ponda Issa Ponda Akiondoka mahakamani mara baada ya kusomewa mashtaka matatu na kesi yake imehairishwa Hadi tarehe 28.08.2013
Ulinzi Ukiwa umeimarishwa mahakamani leo
Sheikh Issa Ponda Akiwa mahakamani mkoani Morogoro asubuhi ya leo Sheikh Ponda Amesomewa Mashtaka Matatu katika Mahakama ya mkoa wa Morogoro Likiwemo la uchochezi alilolitoa Kwenye Mkutano wa Hadhara Tarehe 10 mwezi huu ambapo inadaiwa alisema kwamba ”Ndugu waislamu Msikubali uundwaji wa kamati za ulinzi na usalama za Misikiti kwani kamati hizo zimeundwa na Bakwata ambao ni vibaraka wa Serikali ”katika viwanja vya shule ya kiwanja cha ndege Mkoani Morogoro. Baada ya kusomewa Mashitaka hayo Mahakama imesema Upelelezi Umekamilika na Dhamana Imefungwa na Amerudishwa Rumande Mpaka tarehe 28 mwezi huu ambapo kesi hiyo itaanza kusikilizwa katika Mahakama ya Mkoa wa Morogoro..
Picha Na MATUKIO NA MICHAPO BLOG
Kwa nini Mafaili ya Mtuhumiwa hayakuletwa DSM,mashtaka yakasomewa DSM badala ya kumrusha kwa Chopper(Helikopta) kutoka DSM hadi MRGR na kumrudisha tena DSM kwa Chopper.Wakati mwingine serikali inapoteza pesa bila Sababu za Msingi au sheria hairuhusu?
ReplyDeleteDavid V
naungana nawe!
ReplyDeletehuu ni ufujaji wa pesa ya mlipakodi fukara.
jambo jingine nalaoomba nisaidiwe; kuna yeyete anayeweza kutujuza historia ya huyu bwana!
Aaaa,hata kama historia yake iko namna gani,bado kosa lake si la kuchukuliwa kihivyo,haya yote ni ili kuifurahisha uingereza, cuz the telegraph gazeti la uingereza wanang'ang'ania kuwa ndiye aliye sababisha kumwagiwa tindikali wale waingereza.
ReplyDelete