Watumishi wa Mungu Christina Shusho na Upendo Kilahiro, mwishoni mwa wiki hii watahudumu katika jiji la Washington DC na Vitongoji vyake (DMV).
Shusho na Kilahiro ambao ni miongoni mwa waimbaji mahiri wa muziki wa Injili Afrika Mashariki, wameshawasili Washington DC tayari kwa huduma hiyo ambayo ni sehemu siku tatu za Maadhimisho ya miaka mitano ya kanisa la The Way Of The Cross Gospel Ministries.
Maadhimisho haya yataanza siku ya Ijumaa na kumalizika Jumapili
Maadhimisho haya yatafanyika
The Way of the Cross Gospel Ministries
(at University United Methodist Church)
3621 Campus Drive
College Park, MD 20740
Hii inakuwa ni mara ya pili kwa watumishi hawa kuhudumu pamoja kanisani hapo katika kipindi cha miaka miwili, ambapo mwaka 2011waliungana na Upendo Nkone kuhudumu katika Mkutano mkubwa wa Injili ulilofanyika kanisani hapo.
Watazame na kuwasikiliza wanavyoelezea siku hizo
jamani nimependa sana sana sana tangazo lenu yani Christina Shusho unawezea sana na unaweza kuwa mtangazaji mzuri na pia ukirudi Tz kipaji chako kitumike kwenye matangazo hapa nchini Tz. Mmpedeneza sana na tangazo zuri mnoo, very simple na linavutia nimewasikiliza mara tatu hata sitaki kumaliza. Swali dogo tu vipi safari hii mmemuacha wapi Upendo Nkone? Mbona 2011 mlikuwa wote hapo sasa hivi je? Haya Mungu azidi kuwabariki katika kuifanya kazi yake.
ReplyDelete
ReplyDeletepamenifuraisha hapo mwishoni mtumishi shusho please upendo is doing superb job so as you. you all look beautiful. we had a good time here in houston so i want to encourange everybody in washington dc to go to see how these two sisters use their god given talent to praise God.