Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi,Windhoek Namibia.
Hatimaye timu ya Jeshi la Polisi Tanzania inayoshiriki Michezo ya Nane ya Umoja wa wakuu wa majeshi ya Polisi kusini mwa Afrika (SARPCCO) nchini Namibia imefika salama na imeanza mazoezi mepesi kwa ajili ya kujiandaa na mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza jumatatu tarehe 19 mwezi Agosti mwaka huu.
Timu hiyo ambayo ni tishio katika michezo hiyo kutokana na historia yake ya ushindi katika mashindano yaliyotangulia imekuwa kivutio kila inapopita huku kila mmoja akitaka kusalimiana nayo.
Timu hiyo inaundwa na wanamichezo 67 ambao wanacheza Mpira wa miguu wanaume, Mpira wa pete Wanawake, Riadha wanaumwe na wanawake na mchezo wa Vishale (Dats).
Michezo hiyo itashirikisha Nchi kumi na nne (14) katika michezo mbalimbali na lengo la michezo hiyo ni kujenga ushirikiano wa Majeshi ya Polisi kwa nchi wanachama wa SARPCCO katika kukabiliana na uhalifu.
timu ya Jeshi la Polisi Tanzania inayoshiriki Michezo ya Nane ya Umoja wa wakuu wa majeshi ya Polisi kusini mwa Afrika (SARPCCO) nchini Namibia,wakipiga jalamba wakati wa kujiandaa na mashindano hayo.
Timu ya Jeshi la Polisi Tanzania inayoshiriki Michezo nchini Namibia ikiwa kwenye picha ya pamoja na Baadhi ya Wenyeji wao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...