Bi. Prisca George (kulia) mkazi kutoka Tegeta, Dar es Salaam, anahesabu kitita cha mpoko alichopokea kupitia mradi wa MWEI unaoendeshwa na kampuni ya Vodacom Tanzania. Bi. Prisca ni mmoja wa wanawake wajasiliamali 150 waliopokea mikopo isiyo na riba ya jumla ya millioni kumi kupitia mradi wa MWEI eneo ya Tegeta ili kuendesha biashara zao. Kulia ni Bi. Grace Lyon, Meneja wa Mradi wa MWEI na katikati ni Bi. Zawadi Bakari, wakala wa M-Pesa.
Bi Zaituni Abdalla (kushoto) mkazi kutoka Tegeta, Dar es Salaam, anahesabu kitita cha mpoko alichopokea kupitia mradi wa MWEI unaoendeshwa na kampuni ya Vodacom Tanzania. Bi. Zaituni ni mmoja wa wanawake wajasiliamali 150 waliopokea mikopo isiyo na riba ya jumla ya millioni kumi kupitia mradi wa MWEI eneo ya Tegeta ili kuendesha biashara zao. Anayeshuhudia ni Bi Rukia Mtingwa, Meneja Mawasiliano Vodacom Tanzania.
Bw. Martin Kiswaga (kulia) ofisa kutoka kampuni ya Vodacom Tanzania, akielezea kikundi cha wanawake wajasiliamali kutoka Tegeta, Dar es Salaam, jinsi chaja ya ReadySet inavyofanya kazi. Chaja hio ilizinduliwa na kampuni ya Vodacom na inatumia nishati ya jua kuchaji simu kumi wakati mmoja. Wanawake hao pia walipata mikopo isiyo na riba kupitia mradi wa MWEI ya ujumla ya million kumi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...