Mbunge wa Ilala Mhe Mussa Azzan Zungu (katikati), akizungumza wakati wa kufungua semina ya viongozi wa Ligi kuu na Daraja la Kwanza leo kwenye uwanja wa Taifa.Kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu (DRFA), Almas Kassongo na kushto ni Katibu mkuu wa DRFA Msanifu Kondo.
MBUNGE wa Ilala Mussa Azzan Zungu leo amefungua semina kwa klabu za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara kwa Mkoa wa Dar es Salaam na kusema uchawi katika mpira hakuna.
Zungu alisema hayo wakati akifungua semina hiyo ya siku moja iliyoandaliwa na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) iliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Alisema mpira unataka maandalizi mpira wa miguu unahitaji maandalizi na pesa na kwamba pia unahitaji ghrama kubwa ili kuuendesha.
“Miaka ya nyuma tulikuwa tukicheza mpira kienyeji ingawa kulikuwepo na sheria 17, sasa msione wale wanaoshindwa kucheza hawajui, tatizo hawajawekeza na ndio maana washuka madaraja,” alisema.
Zungu pia alitumia fursa hiyo kumpongeza nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kwa kutojisikia na kuhudhuria semina hiyo licha ya uchovu wa mechi ya jana ya Ngao ya Hisani dhidi ya Azam walioshinda bao 1-0.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa DRFA, Almas Kassongo alisema bado ataendelea kupambana na kutowaangusha wadau wa mpira wa miguu Mkoa wa Dar es Salaam.
“Nipo katika mapamabano ya mpira kwa muda mrefu na nitahakikisha timu mojawapo ya Dar es Salaam inaendelea kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...