Kampuni ya simu za mkononi
ya Airtel imekabidhi Kitengo cha Usalama Barabarani kiasi cha
shilling milioni 40 katika kuhakikisha elimu kuhusu usalama barabarani
inatolewa ili kuthibiti idadi ya ajali za barabarani nchini.
Hundi hiyo imekabidhiwa na meneja mawasiliano wa Airtel Jackson
Mmbando kwa mkuu wa wa Kitengo cha Usalama Barabarani Mohamed Mpinga
mbele ya waandishi wa habari katika ofisi za makao makuu za Usalama
Barabarani.
Kutangazwa kwa ushirikiano huo ambapo Mkuu wa kitengo cha usalama
barabarani Tanzania Kamanda Mohamed Mpinga ametangaza wiki ya nenda
kwa usalama barabarani ya mwaka huu itakayozinduliwa rasmi siku chache
zijazo huko mkoani Mwanza.
Akiongea wakati wa halfa hiyo mkuu wa Kitengo cha Usalama Barabarani
Mohamed Mpinga alisema
”Nachukua fursa hii kuwashukuru wadhamini wakuu
wa kampeni ya usalama barabarani kwa mwaka huu kampuni ya simu za
mkononi ya Airtel, kwa kutoa mchango wao wa pamoja na kushirikiana na
jeshi la polisi usalama barabarani kufikia malengo kwa kuhakikisha
usalama wa raia na kupunguza ajali za barabarani.
”
Ajali za barabarani zinaongezeka kwa kasi na kusababisha upotezaji wa
nguvu kazi huku zikiacha maafa makubwa kwa taifa, ni jukumu la kila
mtanzania kuwa sehemu ya kusimamia na kuzingatia sheria za barabarini
huku tukiishi na kutimiza kauli mbiu ya mwaka huu.
“Usalama Barabarani
unaanza na mimi wewe na sisi sote”.
Nachukua fursa hii kuwaaasa watumiaji wa vyombo vya moto kupeleka
magari yao kukaguliwa na kuthibitishwa ubora wa kutembea barabarani
ili kuhakikisha vyombo vinavyotumika kubeba abiria viko salama na
vinakidhi viwango vilivyowekwa kuhakikisha usalama barabarani.”
aliongeza Mpinga
Akiongea kwa niaba ya Airtel, meneja mawasiliano wa Airtel Jackson
Mmbando alisema “kwa muda wa miaka mitano sasa Airtel tunajivunia kuwa
sehemu ya juhudi za kuokoa maisha ya watanzania na mali zao na tunayo
dhamira ya kuhakikisha tunashirikiana na wadau wote wenye wito wa
kusaidia usalama barabarani na jeshi la polisi usalama barabarani
kupunguza ajali za barabarini kwani moja ya dhamira ya Airtel ni moja
kati ya shughuli za kijamii tunazozifanya nchini.
" Nia na madhumuni yetu makubwa ni kusaidia shughuli zinazofanywa na
jeshi la polisi kusimamia na kupunguza matokeo ya ajali za barabarani,
kila mwaka kunakua na matukio ya ajali za barabarani ambazo zingeweza
kuepukika kama wahusika wangekua na elimu ya kutosha.
"Hii ndio sababu
kubwa na madhumini ya Airtel kuwa mmoja wa washiriki wakuu katika
kusaidia kuhamasisha na kutoa elimu itakayofanikisha upungufu wa ajali
barabarani kwa muda wa miaka mitano sasa.”.
Airtel kwa mwaka huu imechangia kuchapisha stika, kutoa elimu kwa
kwa waendesha Boda Boda , mashindano ya mpira kuhamasisha vijana
pamoja na kutoa vitu mbalimbali ikiwemo T shirt 500 zenye ujumbe wa
mwaka huu “Usalama Barabarani unaanza na mimi wewe na sisi sote”.
Tunaamini ajali za barabarani zinaweza kuepukika ikiwa kila moja
atafanya sehemu yake Mmbando aliongeza.
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani, DCP Mohamed Mpinga (kushoto) akipokea hundi ya shilingi milioni 40 kutoka kwa Meneja uhusiano wa Airtel, Bw. Jackson Mmbando. Hundi hiyo ilitolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa dhumuni la kudhamini wiki la nenda kwa usalama barabarani linalotegemewa kuanza wiki ijayo. Anaeshuhudia kushoto ni kamanda msaidizi usalama barabarani Bw, Johansen Kahatano
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani, DCP Mohamed Mpinga akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kupokea hundi ya milioni 40 iliyotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa dhumuni la
kudhamini wiki la nenda kwa usalama barabarani litakaloanza wiki ijayo.
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani, DCP Mohamed Mpinga akizungumza
Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando akiongea na wanahabari muda mfupi baada ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni 40 kwa Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani, DCP Mohamed Mpinga. Airtel ilikabidhi
hundi hiyo kwa dhumuni la kuendelea kudhamini wiki la nenda kwa usalama barabarani kwa mwaka wa tano mfululizo.
sasa ndio ule muda wa kununua zile stika sio? mimi mpaka leo najaribu kuelewa dhumuni la zile stika bado sipati mantiki yake maana tunauziwa tu mtaani kama njugu bila hata kuonyesha gari husika. Kama ni aina ya kodi basi nanyi mngeiunganisha kwenye leseni ya barabarani kama wenzunu wa zimamoto.
ReplyDelete