Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera , akifungua jengo la Kompyuta la Chuo cha Uuguzi Berega.
Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( watatu kutoka kulia ) walioketi ,
akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Elias Tarimo ( wapili kutoka kulia)
pamoja na baadhi ya viongozi wa Kanisa la Anglikana Jimbo la Morogoro ,
viongozi wa Chuo cha Uuguzi cha Berega , wanafunzi wahitimu wa Diploma
na Cheti , mara baada ya kuwatunuku vyeti vyao Septemba 6, mwaka huu kwenye mahafali ya kwanza ya Chuo hicho
Baadhi
ya wahitimu wa uuguzi na ukunga wa ngazi ya Diploma pamoja na Cheti
kutoka Chuo cha Uuguzi cha Berega , kinachomilikiwa na Kanisa la
Anglikana Jimbo la Morogoro wakila kiapo chao cha kuwauuguzi baada ya
kuhitimu masomo yao Septamba 6 mwaka huu.
Baadhi ya waalimu wa Uuguzi na ukunga wa Chuo cha Uuguzi cha Berega , wilayani Kilosa wakiwa na nyuso za furaha.
CHUO CHA UUGUZI BEREGA KANISA LA ANGLIKANA CHATOA WAHITIMU WA KWANZA .
Picha na Habari na John Nditi).
CHUO
cha Uuguzi cha Berega kilichopo Wilayani Kilosa, Mkoa wa Morogoro na
kumilikiwa na Kanisa la Anglikana Tanzania, Dayosisi ya Morogoro,
kimetoa wahitimu wake wa kwanza tangu kuanzishwa kwake mwaka 2010
katika masomo ya Stashahada ( Diploma ) na Cheti
Katika
mahafali hayo ya kwanza yaliyofanyika Septemba 6,mwaka huu ambapo mgeni
rasmi alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera , jumla ya
wahitimu 22 walitnukiwa vyeti vyao kati yao 13 ngazi ya stashahada (
Diploma ) ya miaka mitatu na wengine tisa ngazi ya cheti , ambapo mwaka
huu jumla ya wanaunzi 53 wamejisajili kati ya hao 25 ni wasichana na 28
wavulana.
Jamani basi , kwa kuwa mmeelimika washawishi wenzenu waache kutusi akina mama wanaoenda hospitali kujifungua.
ReplyDeleteHasa wauguzi wa kike.