WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kuhakikisha inaisimamia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kuhakikisha kuwa wanagawa chakula cha bure kwa kaya 20,000 zinazoishi katika Tarafa ya Ngorongoro.
Ametoa agizo hilo jana jioni (Alhamisi, Septemba 19, 2013) wakati akizungumza na wakazi wa kata saba za Tarafa ya Ngorongoro katika mkutano wa hadhara uliofanyika Enduleni Madukani wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
Waziri Mkuu ambaye yuko mkoani Arusha kwa ziara maalum ya kusikiliza matatizo ya ardhi yanayowakabili wakazi wa wilaya ya Ngorongoro, kabla ya kuhutubia mkutano huo aliamua kukutana na Baraza la Wafugaji pamoja na wazee wa kimila (Malaigwanan) na kusikiliza kero kutoka kwa wazee hao.
Kero kubwa iliyowasilishwa kwenye kikao cha Malaigwanan na kwenye mkutano wa hadhara wa Endulen, ililenga kuiomba Serikali iwape ruhusa ya kuwa na mashamba madogo ya kujikimu kwenye maboma ya wafugaji wa Kimasai wanaoishi kwenye Hifadhi ya Ngorongoro. Kero nyingine zilihusu ukosefu wa maji, ajira wa vijana, mitandao ya simu za mkononi na upatikanaji wa chakula cha msaada kwa haraka.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...