NA Ibrahim Kamwe 'Big Right'

Asili ya mabondia wengi  duniani wanatoka katika familia duni kwa mfano hapa kwetu Dar es salaam ni mara chache kumkuta bondia ametoka Upanga, Oysterbay, au Masaki ushuwani, nikiwa na maana  mabondia wengi wanatoka uswahilini na ni watu wa hali duni kimaisha, ambapo wengi wetu hatujakalia madawati ya shule ama wengine tuliojitahidi tumefika darasa la tano au sita; kama wazazi walikomaa ndio tunamaliza la saba. 

Baadhi yetu tukiwa na umri wa kuanzia miaka sita nyumbani huwa tunaanza kupewa uzowefu wa kuuza visheti,maandazi, vitumbua, karanga n.k.  na vikibaki nyumbani hauli chakula mpaka viishe. Shuleni mwalimu mkali balaa, darasani hafundishi mpaka usome tuisheni kwake ndio unapata kufundishwa kidogo na ukishindwa maswali yake unakula viboko vya ghadhabu ,hapo ndipo tunapoamua kuachana na shule na kutinga mitaani.  

Michezo yetu ni katika madampo na vichochoroni na tukifikia umri wa kuanzia miaka 12 na kuendelea tunajua jinsi ya kutafuta pesa kwa kuuza njiwa,kucheza kamari,malani,kuiba kuku na bata. Kwa wale walio watukutu zaidi kuuza na kuvuta bangi ni sehemu ya maisha ya kawaida tu huku mitaani kwetu. Aghalabu mlo kwetu ni mmoja tu kiubishoo au kuna wageni nyumbani ndio tunakula milo miwili. 

Katika maisha yetu muda mwingi tupo huru na michezo kuliko kusoma hasa kolokolo,ngoma,mpira na ngumi, mpira tunacheza mabarabarani ,vichochoroni na madampo wakati ngumi tunajifundisha katika makamali vichochoroni au uwani kwa kina masta, begi au tairi limefungwa juu ya  mti tizi linaendelea bila vifanyio vya mazoezi vilivyo rasmi mwendo mdundo tunasonga na tunashinda au kufanya vizuri  katika mashindano yetu tunayoshiriki na hali yetu duni hihi hii ya kimaisha, na majina yetu kutangazwa sana katika vyombo vya habari na kupata umaarufu mkubwa nchini,nchi jirani  na hata nchi za ulaya. Lakini ukibahatika kututembelea na kuangalia tunapoishi na familia zetu na umaarufu tulionao na maisha yetu mabovu inasikitisha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Huu ni mchezo wa wasio akili.Kwanza fikiria katika dunia hii huu ni mchezo unapoingia jukwaani una nia ya kumdhuru unayecheza naye. You want to cause him damage deliberately.Kisha wapewa taji la maua, na wenye faida ni wale wanaovaa suti na kukuangalia wewe ubongo wako wakorogwa.This "game" should be banned,its primitive. But it wont because there are those clever ones who have powerful lawyers and use them like "milch cows".

    ReplyDelete
  2. Mdau Ibrahi Kamwe 'Big Right',

    Umenena ya kweli kabisa kuwa Tasnia ya Ndondi nchini inabebwa na wale waliopitia maisha ya kupinda!, haishangazi pia tukiangalia Kimataifa kama kule Marekani tunaona alikotokea Mike Tyson ni ktk mazingira a Kimaisha uliyoyasema hapo, hata tukija kwa Miamba wengine wa Magumi haya kutokea Mexico na Cuba wengi wamepitia maisha ya Misoto nafikiri ukiunganisha na Suala la ''Mipango ya Unga'' vinaendana kabisa!!!

    ReplyDelete
  3. yaa hii full adventure yaani, mtoto wa geti hajui hii

    ReplyDelete
  4. hii ni kweli tupu,,,maana hao wapiganaji ngumi,hata sura zao,,Upanga masaki na kote huko uzunguni hazipo.Ni sura za kijambazi jambazi ambazo hazina hata hata aibu nyuso zao.
    Ni kweli kabisa tangu lini wewe mwanadamu ukata kummaliza kabisa binadamu mwenziwe bila hata ya kukufanyia kosa,kisa uvalishwe mkanda na vijisent kidogo...
    Kweli mchezo wa kinyama huwo

    Ahlam London

    ReplyDelete
  5. Mwandishi umenigusa sana na habari ulivyoiandika, yaani nimekua ktk mazingira hayohayo na nimesoma na kufanya biashara hizo hizo za visheti,vitumbua,samaki,karanga ila namshukuru mungu sasa nipo scandinavia nafanya specialization ktk medicine nina mengi ya kuhadithia baadae ili kupeana matumaini,wakati mwengine naweza kusema nimeponea ktk tundu la sindano, vinginevyo hali ingekua mbaya.Kwa kifupi mimi natokea kwa mtogole ebu pata picha mwenyewe.

    ReplyDelete
  6. Kwa wengine kama mimi ni hobby. Kupigana is so natural mpaka wanyama wanapigana, hujawahi kuona simba au chui wanacheza mpira. This is a natural sport. Ni kweli most of the time is fight for survival and katika umasikini wetu people take advantage. Michezo yote bongo sio deal mwishoni unaishia masikini. Natoa salaams kwa mabondia wooote Tanzania, I wish I can do something for the sport

    ReplyDelete
  7. ni ukweli kabisaa kaka yangu maandishi uliyoandika hapo juu. Wadogo zangu walijitahidi kuingia katika hiyo tasnia, wakashindwa, matoke yake walienda kupaa samaki huko feri. Leo hii wanamiliki hata nyumba na magari, sisi pia tumetokea tandaleee kwa mtogele!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...