Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Padri Joseph Monesmo Magamba, wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui, alipofika katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kumpa pole,Mjini Unguja,baada ya kumwagiwa tindikali na watu wasiojulikana katika Mtaa wa Mlandege Mkoa wa Mjini Magharibi jana jioni, Padri alimwagiwa Tindikali alipokuwa akitoka kupata huduma ya Mtandao
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimsikiliza Padri Joseph Monesmo Magamba,wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui,akitoa maelezo jinsi alivyopata mkasa wa kutiwa  Tindikali jana na watu wasiojulikanwa,katika mtaa wa Mlandege Mjini Unguja, alipofika katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kumpa pole,ambapo amelazwa na kuapatiwa matibabu.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiwafariji jamaa  na ndugu wa Padri Joseph Monesmo Magamba,wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui,waliofika katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kumpa pole Padri huyo baada ya kumwagiwa Tindikali na Watu wasiojulikanwa jana jioni Mtaa wa
Mlandege Mjni
 
 Mmoja wa Ngugu wa Padri Joseph Monesmo Magamba,wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui,akimueleza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,hisia zake kwa Uchungu kutokana na kitendo hicho cha kumwagiwa Tindikali na watu wasiojulikanwa  kwamba zilichukuliwe hatua za kisheria na kukomeshwa Vitendo kama hivyo

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifafanua jambo wakati akiwafariji jamaa na ndugu wa Padri Joseph Monesmo Magamba,wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui,waliofika kumuangalia Padri huyo aliyelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja baada ya kumwagiwa Tindikali na Watu wasijulikanwa jana jioni katika Mtaa wa Mlandege Mjini Unguja.
Picha na Ramadhan Othman wa Ikulu, Zanzibar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Viongozi mtaendelea kuwatembelea Wahanga wa Tindikali hadi lini?Nadhani wa husika wapewe adhabu ya KIFO kama wale Wabakaji wa India Ili kukomesha kabisa janga hili.
    Hii inawezekana kwa kurekebisha Sheria zilizopo kama walivyofanya India.Kama sikosei hii ni zaidi ya mara Sita kwa viongozi wa juu kwenda hospitali na kupiga picha za namna hii ambazo kwa mtazamo wangu hazisaidii sana.

    ReplyDelete
  2. Tusikurupuke kupendekeza adhabu kwa wale tu wanaomwagia watu tindikali. Hapo tutakuwa hatujatibu ugonjwa. Ni sawa na kuweka plasta tu kwenye mdomo wa jipu, badala ya kutumbua jipu na kutoa uchafu na kisha kufuatilia kwenye damu ni kitu gani kimachafuka kusababisha hilo jipu! Jipu lenyewe ni viongozi wa upangaji wa hayo matukio (wamwagaji hao tu ni watumikaji). Mfumo wa damu ni kuangalia jamii nzima bara na visiwani, kulikoni watu ndugu ghafla kuchukiana kiasi hicho!! Mwenyezi Muumba hakika ametupa akili za kujitafakari na kujua tatizo, tusikimbilie kulaumu tu!!

    ReplyDelete
  3. Viongozi sasa inabidi mkune vichwa, tumefika pabaya.

    Inakuwaje tangu haya masuala ya tindikali yaanze hatujaona wahusika kukamatwa?

    ReplyDelete
  4. Ningependa yule polisi aliyetoa hojambovu kuhusu yule padre aliyeuwawa aseme tena leo. Jambo hilo halikutendwa kinyemela hivyo walioona bila kuchukua hatua nao wameshiriki.Si bure na serikali ya mapinduzi inajua.

    ReplyDelete
  5. Pengine tatizo kubwa hapa si hawa wanaotenda huu uhalifu. Tatizo kubwa ni hii serikali isiyowahakikishia watu wake usalama. Kama mhalifu ana uhakika akitenda tena hatakamatwa, kwa nini asirudie?? Hatuwezi kukomesha uhuni huu bila kuwa na mamlaka inayowajibika. Inakuwaje matukio yote wahusika hawakamatwi, na bado tuna dola inayowajibika??

    ReplyDelete
  6. Jina lake linakosewa sana ni Padre Anselmo Mwang'amba,Mungu amponye haraka na twaiombea serikali yetu ipate hekima ya kuyapatia ufumbuzi matukio haya kabla mwingine hajaathirika na haya tena.

    ReplyDelete
  7. Ndio naungana a mtoa maoni september 14,kwamba tatizo kubwa si si wahalifu bali ni serikali tena Ya Muungano,kwa kuwa Tumeomba katika katiba kuwa Tuwe na Polisi yetu basi naamibi tungeweza kushuhullikia hili tatizo kwa Vile polisi ni Ya Muungano wao ndio wa kuwajibika chenine ni hiki Hawa japo kuwa ni viongozi wwa dini lakini je Hawana matatizo na watu wao ijapokuwa halijahusishwa hili tukio na mambo ya dini juzi tu Christian Msema wa Mburahati, Dar es Salaam kumwagiwa acid na watu wasiojulikana waliokuwamo kwenye bajaj hakuna aliemtembelea lakini ikiwa Kiongozi wa dini mbio mbio ....

    ReplyDelete
  8. Zanzibar kwa Watalii, Viongozi wa Dini, Chama na Serikali wanahitajika kuvaa 'Masks' ktk nyuso zao na Makoti ya 'Nailon' ili kujikinga na mashambulizi ya kumwagiwa Tindikali !!!

    ReplyDelete
  9. Zanzibar,

    Hata nchi hizi za Kiislamu zina wakazi Wakristo pia!

    1.Jamhuri ya Kiislamu ya Iran,
    2.Saudi Arabia,
    3.Pakistan,
    4.Iraq,
    5.Jordan,
    6.Lebanon,
    7.Misri

    Pia mkumbuke ya kuwa Ukristo ktk Afrika ya Mashariki uliingia kupitia hapo hapo Zanzibar kama mnavyoona Kanisa kongwe Afrika ya Mashariki lipo Zanzibar,

    Hivyo hamwezi kuipindisha Historia hiyo!

    Ni lazima mkubaliane na mchanganyiko wa Dini!!!

    Pia muelewe ya kuwa Muamko wa Uislamu hautegemei make pake yanu tu Kisiwani.

    Elimikeni.

    ReplyDelete
  10. Tatizo la hawa wanaomwagia wenzao tindi kali hawana utu wala ustaarabu kwao wanakotoka sio dini,dini ipo Zanzibar miaka yote na hakuwahi mtu hata kutemewa mate kwa kuwa anatoka dini ya kikristo.
    hii mijitu imejaa Zanzibar mjini kazi haina wala elimu ndio mwiko wamezagaa kama dagaa hapa mjini sasa serikali ina kazi ndogo tu ya kuwapeleka makwao vijijini na sehemu yoyote wanakotoka kama vile wanavosafirishwa huko bara wale wanaotoka mikoani hurudishwa vijijini wakalime au wakakae bure hapa Zanzibar iko haja ya kuanza kurudishana mashamba,pemba au uzi n.k.
    kisingizio cha hapa kwetu iwe basi kama huna kazi maalum inayokuweka mjini rudi ulikovunjia ungo au balehe yako hii ishakuwa hatari.
    bila kufanya hivyo hili tindi kali itakuwa ndio poda ya kila mtu mwenye kunuka kwapa.
    kisingizio cha ubaguzi kisitumike kwani kama nilivosema bara wametumia mfumo huu wa kuwasomba somba wazururaji mjini ovyo na kuwarudisha makwao haina maana dar es salaam sio kwao lakini kwa kuwa hawana kazi inyowaweka ndio maana hupelekwa huko ili kusafisha mji.
    Zanzibar amkeni katika huu urojo mnaokunywa mchana sasa mnakunywa tindi kali lakini bado mnafikiria kiurojo urojo shehe wa kiislamu kamwagiwa bwana soroga,sasa padiri, na yule mwingine padiri walimuuwa kabisa, wazungu tayari,sheha wa jangombe bwana kidevu tayari na yule mkurugenzi wa manispaa tayari swali la kujiiuliza bado nani?
    mimi nimeonya zamani mawaziri wa Zanzibar na wawakilishi wote kaeni mkao wa kula tindi kali linakuja sasa zamu yenu kwani ikiwa wanapomwagiwa wengine nyinyi mmekaa kimya subirini msiba uhamie kwenu ndio mtaitafuta dawa kama mnayo.
    mdau.
    Zanzibar.

    ReplyDelete
  11. Mdau wa 9 hapo juu uliyesema nchi zenye Wakristo, hawa wamwagia watu Tindikali zaidi way Wakristo hao huko Arabuni mfano nchi zingine hizo wapo wasio na Dini kabisa!,,,yaani Pagan na Waarabu wanawaita 'MAJUS' ni wengi wanaishi Majangwani.

    ReplyDelete
  12. Angalieni hawa watu wamwaga Tindikali,

    Wewe mmwagaji Tindikali Uislamu wetu huu huu Swala 5 na Nguzo 5 za Uislamu zina kushinda kutekeleza leo unakuja kumuhukumu mwenzio na Dini yake?

    (Naomba Mwenyezi anisamehe kwa matamshi yangu)

    ReplyDelete
  13. This is too much kila kukicha viongozi kwenda kutoa "pole", inasaidia nini? Vipi serekali imeshindwa kuunda kikosi maalumu cha kukomesha huu uhalifu. Unda kikosi maalum cha makachero na ndani yake wawepo informants, ambao ni hao hao wenye siasa kali ambao wanaishia kuwachoma wenzao. Mara nyingi informant ni mtu ambaye analipwa vizuri au mwenye makosa makubwa ya kusotea jela lakini kutokana na kutoa ushirikiano kwa serekali anakuwa huru na kulipwa pia. Napendekeza serekali kuchukua hatua kali kuthibiti uhalifu aina hizi za uhalifu

    ReplyDelete
  14. Mungu baba aukuponye, serekeli mpo ?

    ReplyDelete
  15. Haitoshi kumtembelea mwathirika pekee na kutoa pole, ingafa hapo sasa kiongozi atoe masaa 24 kwa watu wa usalama kuwa wameshawakamata wahusika. Kwa ZNZ ilivyo ndogo wahusika ni rahisi kukamatwa, tena wahusika wa mwanzo wa kuisaidia polisi ni wale waliokuwepo jirani na tukio, nadhani wapelelezi hawako serious na kazi yao.

    ReplyDelete
  16. Huyo mjinga anaesema kama washamba warejeshwe makwao hapo zanzibar katiba ya zanzibar inasema kila mzanzibari ana haki ya kuishi popote pale anapotaka bila ya kubugudhiwa ndani ya zanzibar hiyo sisi hatufanyi mambo kichwa mchungwa mambo hayo ni huko TANGANYIKA ndio wewe ukiwa mshamba ukaishi shamba huna haki ya kuja mjini ukoloni huo mkoloni sio lazima awe mweupe hata wakoloni weusi wapo zanzibar ina sheria na katiba yake na sio kwa sababu mtanganyika mmoja kamwagiwa tindi kali ndio iwe sababu tuvunje sheria zetu na katiba yetu huo upumbavu kuweni na akili na mjuwe ya kuandika na kama mmekasirika zaidi kila mtu ana kwao makwenu mnakujuwa ondokeni zanzibar hapo mmeletwa na njaa zenu ndizo zilizo waleta zanzibar msitupangie sheria kwamba washamba warudishwe shamba rudini nyinyi makwenu IRINGA, SONGEA what ever yuo FUCKING COME FROM hamkulazimishwa kuja zanzibar njaa yenu ndio zilizo waleta hapo msianze kutupangia sheria za kuvunja katiba yetu na sheria zetu za SMZ.

    ReplyDelete
  17. waambie tena wasikie warudi makwao hatwataki mumejaa natuta fanya juu chini mutaondoka kama mulivokuja musitake munahaki ndani ya zanzibar hamuna jifanyeni wanyonge lakini nyinyi waongo muna malengoyenu na wallahi sumawallahi hamuto fanikiwa mutateseka mpaka mutatuachia tupumuwe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...