Kwanini ? Vibali vyote vya kuishi wageni visifutwe na kusajiliwa upya.
Msako lazima uwe na kasi kubwa tena uanzie mji mikubwa kama Dar,Arusha...

Kuanzia mwezi julai 2013 kiongozi mkuu wa nchi yetu rais Dk.Jakaya Kikwete katoka agizo kuwa raia wote wa kigeni ambao ni wahamiaji haramu wamepewa siku 14,kuondoka au kujisalimisha katika vyombo vya dola.

Agizo hili la rais lina lengo zuri tu kwa watanzania na usalama wa watanzania,lakini utekelezwaji wake umekuwa hauna kasi,kwani idadi ya wahamiaji haramu walio jisalimisha ni ndogo kulingana na waliopo nchini,na kati ya hao walijisalimisha ni wahamiaji waliopo nje ya miji mkubwa sio katika miji mikubwa kama Dar ,Arusha na
kwingineko !

Cha kushangaza kwamba kuna baadhi ya wahamiaji haramu au halali wanakiuka kwa namna moja au nyingine sababu zinazowafanya kuwepo nchini Tanzania.

mfano raia wa kigeni aliyekuja nchini kwa kufanya kazi fulani na akapewa kibali kwa ajili hiyo anakiuka kwa taratibu za uhamiaji na kuanza kuwa mfanyi biashara ya baa au dangulo fulani! au pengine kujiingiza katika biashara ambayo mzawa anaweza kuifanya, na huku vyombo vya usalama vikimwangalia !

Hivi kuna uhalali wa kisheria Raia wa kigeni asiye na hata asili ya Tanzania kumiliki nyumba au Ardhi ?

Watanzania wengi wamekuwa wakilalamika juu ya ongezeko la raia wa kigeni hususan raia wa nchi za ulaya,Asia na nchi za kiarabu kumiliki au kununua nyumba na ardhi nchini ,mfano wachina wanamiliki majumba au ardhi uenda wakawa wanakiuka sheria fulani za nchi,na watanzania wanao wauzia nyumba wageni hao nao pia wanajisaliti au kuisaliti nchi.

Ukiwikaji wa sheria za ajira ! mchina anapofanya ya kuuza duka na mitumba au kubeba zege !  Mzungu anapokuja kutalii na baadaye 
kupata ajira ya muhudumu wa hotel ! hili nalo neno?
Bendi za muziki zinapo ajiri wanenguaji kutoka nje ya nchi!

Ndio maana watanzania walio wengi wanaona kuwa hipo haja kwa serikali
kuvifuta vibali vyote vya wageni na kuanza zoezi la kuvitoa upya na kuvihakiki kwa kupitia Wizara ya mambo ya ndani.

Kama Rais JK kesha toa agizo tangu mwezi julai mbona utekelezaji wake
una mwendo wa pole ? wakati kiongozi mkuu wa nchi,ambaye ndiye amri
jeshi mkuu kishaagiza siku 14 tu kila muhamiaji haramu aondoke sasa
tena msako kwanini? usianze katika kutekeleza agizo la mkuu wa nchi.

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Mbariki Rais JK

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Sawa mdau tupo pamoja,tena hili agizo la Rais limekuja muda muafaka,coz kunavitambulisho vya TAIFA vishaanza kutolewa sasa hata hapa wahamiaji haramu nao wajipenyeze kupewa hivyo vitambulisho ndugu zangu watanzania sote kwa pamoja tuseme no no and no ili tuliokowe TAIFA letu,tuliokoe kivipi? Bc mm na nyinyi kwa pamoja tuwasaidie Polisi,emigration au wizara ya mambo ya ndani,idara ya vitambulisho vya Taifa au NIDA,bila ya kusahau Usalama wa Taifa,so tuwasaidie kuwafichuwa kwa majina WAHAMIAJI HARAMU WOTE,unapofanya kazi ukijua huyu mgeni bc tonya mwanangu ilituokoe Taifa letu,angalizo hili jukumu ni letu sote tuilinde NCHI kwa pamoja bila kuchoka,mitaani tunako ishi usije nambia HATUJUANI? Sito kuelewa,mbinu ni zile zile za enzi ya NYERERE (RIP) watanzania tunajuana kwamacho,mwendo,nakupitia kwa WAJUMBE WA NYUMBA KUMI,ndugu zangu mm naitwa MDUDU KAKAKUONA mwenye macho ma3,huo ndio ushauli wangu ili tuliokowe Taifa letu,nakuombeni ndugu zangu chonde chonde na nyinyi mnisaidie kuleta MAWAZO YENU,kumbukeni hii ni VITA ya KUIKOMBOA NCHI YETU,mm niko huku UK au UINGEREZA naona wenzetu huku wanavyoilinda NCHI YAO,

    ReplyDelete
  2. Sifikiri kama kuna wageni wanataka kuja TZ kupiga box. Sijui wataanzia wapi?

    ReplyDelete
  3. Ni kweli kabisa inabidi tulinde maslahi ya nchi na wananchi kwanza.
    Huko Ulaya na Marekani kuanzia sasa hata kama una vibali ukikamatwa unaendesha gari ukiwa umelewa kwa mara tatu tu wanakufutia hicho kibali.
    Ukipigana(kumpiga) na mkeo nyumbani kwako pia unafutiwa kibali.
    Ukiwa mwizi ,jambazi nk unafutiwa kibali.
    Kuanzia sasa hupewi leseni ya kuendesha gari kama huna kibali hupewi,ndio maana wengi wanarudi nyumbani wenyewe.

    ReplyDelete
  4. Wageni wengi kutoka Asia na Ulaya wanajihusisha na biashara haramu ,haswa madawa na ngono(madanguro).
    Wanamiliki majumba ya starehe (bar,pub nk) kuweza kujificha kwenye kivuli huku wanaendeleza uharamia wao.

    ReplyDelete
  5. Mdau unayesema hudhani kama mtu anaweza kujan Tanzania kupiga box nakuona wewe ni mtu wa ajabu na unye idharau nchi yako.Kwa taarifa yako watu wengi wanalilia kuja kufanya kazi na kuishi Tanzania kwani kuna utajiri mwingi sana ambao wewe na wjinga wengine hamuujui ndiyo maana kila mtu ajitahidi hata kwa magendo apate pasi ya Tanzania. Idadi ya Watanzania waishio nje ya nchi ni ndogo sana ukilinganisha na wageni waishio Tanzania

    ReplyDelete
  6. Tunaunga mkono ombi lako ila watu wetu wanapenda sana rushwa ni ni warahisi sana kudanganywa. Hii ni changamoto.

    ReplyDelete
  7. Mtoa Maoni wa No. 2,

    Bongo Tambarale babake!

    Hivi sasa Bongo na Majuu tofauti hakuna!

    Wewe ukifikiri hakuna atakaye kuja kupiga Box Tanzania unaona wanao fukuzwa wanatoka wapi?

    Inawezekana ktk hao Wageni haramu wamo Wazungu wanaotokea kwenye nchi uliyopo wewe!!!

    Kalaga baho!

    ReplyDelete
  8. Wageni Haramu wana maafa makubwa sana kuliko faida.

    Kwa uchache ni:

    1-Uhalifu,
    2-Uhujumu wa Uchumi,
    3-Matatizo ya Kijamii,
    4-Uharibifu wa Mazingira,
    5-Wanaua kasi ya Maendeleo,

    ReplyDelete
  9. Tupo pamoja, Zoezi la kuondoa wahamiaji haramu lifanyike haraka sana, lah nao pia watapata vitambulisho. Kwa mfano maeneo ya City Centre, Kariakoo kuna wahamiaji kibao hasa Wachina, Wasomali n.k. Kwa jirani zetu hapo waliwafumbia macho wakati wanahamia mpaka wameshaenea sehemu kubwa na kuleta usumbufu na wanadai haki sawa kama raia; wakati nchi yao wameiharibu na haina amani wala serikali mpaka sasa. Kama na sisi Watanzania tutawaacha watazidi kuletana, hata kiswahili hawajui.

    ReplyDelete
  10. Wakati hilo linatekelezwa, nadhani pia nature yetu watanzania tunazingatia utu wa mtu na maadili yetu. Good reasoning pia itumike. Nimesoma Nipashe leo, mzee wa miaka 75 ambae alikuja Tanzania 1976, yaani miaka 37 iliyopita na akiwa ameoa mtanzania, na watoto, aliwekwa katika listi ya wanaotakiwa kurudishwa Rwanda. Kupinga hilo yule mzee akajinyonga. Mama hajulikani yuko wapi, watoto na familia nzima imesambaratika, na baba wamemkosa pia. Sielewi kama it makes sense kwa mtu ambae amekaa muda wote huo, na hajavunja sheria yoyote kwa nini awekwe sawa na wengine? Huyo by definition ni mtanzania tu, ukimrudisha Rwanda given his age, na baada ya miaka yote hiyo, unategemea ataanzaje kuji-establish?? Watu kama hao wanalitakiwa kupewa uraia tu. Sijui wahusika wanajifunza kutokana na matukio kama haya angalau wayaangalie upya.

    ReplyDelete
  11. Anony hapo juu, kama mtu amekaa nchini muda wote huo kwa nini hakuomba uraia wakati sheria zipo wazi? Kuna nchi za wenzetu hawataki kupoteza identity yao, kama wanang'angainia hivyo basi wasitulaumu inabidi wachague moja!!

    ReplyDelete
  12. serkali mje Freedom electronics muone wahindi wanavyolipwa dola bila kibali na maofisa wanavopitia posho....mje kaa nje mlangoni hesabu wahindi wanaoingia angalia kazi anazofanya................

    ReplyDelete
  13. E bwana eh!
    Hivi wabongo tunasema tunatania?
    Eti hivi sasa bongo na majuu hakuna tofauti!
    Mama yangu!
    Tofauti ipi hiyo mdau anayoizungumza?
    Matibabu? Usafiri? Umeme? Polisi? Barabara? Shule? Usalama? Mshahara? Usafi? Mipango miji? Ni tofauti ipi hiyo ndugu yangu mdau?
    Unajua hatari ya ujivuni usio na sababu ni kupelekea wananchi kubweteka.
    kamwe huwezi kutamka bongo na majuu hakuna tofauti.
    siku nilipokwenda Bujumbura nikatamani baadhi ya mambo tungeiga kutoka kwao.
    Nilipopita Cairo airport nikatamani Dar au Mwanza au Zanzibar nako kungekuwa na uwanja kama ule.
    Kwa mtanzania kudai bongo kama majuu ni kujirudisha nyuma.
    Acha kwanza tujaribu kukwea vichuguu ndipo tukiweza tutafakari kujiandaa kupanda mlima.
    Wala hapa lengo langu si kuibeza bongo. Bongo ni kwetu na nakupenda zaidi kuliko hapa ugenini ninapoishi. Ila sina budi nikiri kuwa ukweli ni kwamba kamwe nchi ya dunia ya 3 hailinganishwi na ya kwanza.
    Tusijipweteke tukadhani tushafika. Safari ni ndefu. Twendako ni mbali kuliko tutokako.
    Mndengereko Ukerewe

    ReplyDelete
  14. Mdau wa Pili juu No.2

    Kimbunga cha Kwanza ni Wageni haramu nchini Tanzania, na Kimbunga cha Pili ni kuwakusanya ninyi Mnaoishi Majuu bila Sheria kwa kazi za kubeba Maboxi

    Mnaiaibisha nchi hivyo JK ataelekeza nguvu huko kuhakikisha wooote mnarudi Tanzania!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...