Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz akionesha bunduki iliyokamatwa mbele ya waandishi wa habari(hawako pichani)inayodaiwa kutumika katika mauaji ya bilionea wa madini Erasto Msuya.
 Bunduki inayodaiwa kutumika katika mauaji hayo.
Pikipiki mbili zinazodaiwa kutumika katika mauaji ya bilionea wa madini Erasto Msuya.


Picha na Habari nan Dixon Busagaga 
wa Globu ya Jamii, Moshi.

JESHI la polisi mkoani Kilimanjaro limefanikiwa kunasa bunduki aina ya SMG yenye namba za usajili  KJ10520  inayoaminika kutumika katika mauaji ya mfanyabiashara bilonea wa madini ya Tanzanaiti , Erasto Msuya (43) aliyeuawa kwa kupigwa risasi 13 kifuani Augosti 7 mwaka huu Mijohoroni wilayani Hai.

Mbali na bunduki hiyo jeshi hilo pia limefanikiwa kuwatia mbaroni watuhumiwa wengine wanne wanaodaiwa kuwa ni watuhumiwa muhimu katika mipango ya mauaji ya mfanyabiashara huyo anaye aminika kuwa na vitega uchumi vya kutosha katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.

Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake,kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro,Robert Boaz,aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni ,Sadick Mohamed Jabir(32) mkazi wa jijini Dar es salaam na Lang’ata
wilaya ya Hai na Karim Issa Kihundwa(33) mkazi wa Lawate wilayani Siha ambao wanatajwa kuwa ni muhimu katika mauaji hayo.

Alisema watuhumiwa hao wawili walikamatwa  eneo  la Kaliua wilaya ya Sikonge mkoani Tabora wakiwa kwa mganga wa kieneyeji wakifanyiwa zindiko ili wasitiwe mbaroni  na baada ya kuhojiwa na polisi walieleza jinsi walivyoshiriki mauaji hayo na mahali walipoficha silaha na pikipiki zilizotumika katika tukio hilo.

Boaz aliwataja watuhumiwa wengine kuwa ni Jalila Zuberi  Said(28) mkazi wa Babati mkoani Manyara pia anaishi wilaya ya kondoa mkoani Dodoma na Joseph Damas Mwakipesile maarufu kwa jina la ‘Chusa’(35) ambaye pia ni mfanayabiashara wa madini ya Tanzanite anayeishi Jijini Arusha ambaye anashikiliwa na jeshi hilo kwa zaidi ya wiki mbili sasa.

Alisema jeshi hilo pia limefanikiwa kukamata pikipiki nyingine inayodaiwa kutumika katika tukio hilo yenye namba za usajili T751 CKB aina ya KINGLION rangi nyeusi  ambayo wakati wa tukio ilikuwa ikitumia namba za bandia.

Kamanda Boaz alisema Bunduki iliyokamatwa ilikutwa ikiwa imefichwa kwneye tindiga katika eneo la Boroi kwenye mpaka  wa wilaya za Hai na Siha huku akiendelea kutoa  wito kwa wananchi wapenda  amani mkoani Kilimanjaro,kuendelea kutoa ushirkiano kwa jeshi hilo katika kukomesha uharifu.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Ni kwa nini RPC ameharibu kesi hii nzuri?Kwa nini asingetumia latent gloves kushika bunduki ili kuhifadhi vielelezo muhimu(yaani alama za vidole-finger prints).Ni watu wangapi sasa watakuwa washika bunduki hiyo pamoja na pikipiki,lo,nasikitika sana!Uharifu hauwezi kupungua au kuisha katika mazingira haya.Ikumbukwe washukiwa watawekewa mawakili kwa gharama za serikali,haoni kwamba watashinda kesi hii kwa kuwa vielelezo muhimu vimeondolewa?Washukiwa wanaweza kupatikana na hati mahakama kuu,lakini wakashinda kesi kupitia rufaa.Ni mpaka lini polisi watabadilika na kuwa makini katika handling exhibits?Kukamata washukiwa na vielelezo ni kazi yao ya msingi,hivyo hawana haja ya kuonyesha,na kama watafanya hivyo,tahadhali tangu ukamataji mpaka kuonyeshwa vielelezo hivyo lazima ichukuliwe kwa umakni mkubwa sana.Naomba wabadilike ili waharifu waadhibiwe kama wanavyostahili.Mwenye mawasiliano na RPC wamjulishe kuwa ameharibu kesi.

    ReplyDelete
  2. Aisee mimi mwenyewe nimeshangaa sana!Shocking how he is tampering with evidence.

    ReplyDelete

  3. me ningependa kujua motives za hawa majambazi sasa walimuua kisa hela peke yake au kuna kingine??

    alafu mnaposema billionaire wa arusha hivi alikua listed forbes kama billionaire ama wapi?? kuna quaities za kuna billionaire jamani sio kutaja tuu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...