Mwezeshaji wa warsha Bw. Mwalimu Wilson-olesira alie simama akizungumza na washiriki wa warsha ya kujadili mchango wa jamii katika kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu, katika ukumbi wa zamani wa Radio uliopo Rahaleo Mjini Zanzibar. Warsha hiyo ya siku 1 imeandaliwa na (ZAPHA +).
Afisa vituo vya kulelea watoto yatima Idara ya Ustawi wa Jamii Zanzibar Lahdad Haji Chum akichangia katika mjada wa nini tufanye kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na (ZAPHA +) katika ukumbi wa zamani wa Radio Zanzibar.
Maryam Charles Samwel mmoja ya vijana wanaosaidiwa kimasomo na (ZAPHA +) akizihamasisha Jumuiya nyengine kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu magumu katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na (ZAPHA +) katika ukumbi wa zamani wa Radio Zanzibar uliopo Rahaleo Mjini Unguja.
aadhi ya washiriki wa warsha ya siku moja iliyo jadili mchango wa jamii katika kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu, huko katika ukumbi wa zamani wa Radio Zanzibar uliopo Rahaleo Mjini Unguja. (Picha na makame Mshenga-Maelezo)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...